Ahoua Jean Charles usajili bora zaidi Tanzania

Sajili za makolo huwa ni za mihemko tu ngoja ngoma ianze tutayaona yale yale ya kina Fred na Jobe!

Nafasi ya tatu ndio inapendeza zaidi kolokoloni kwasasa!
Maisha yanabadilika Mkuu. Haya maisha ya kuamini timu pinzani ni ile ile ni moja ya Sababu ya Yanga kuwa bora zaidi ya Simba miaka mitatu iliyopita.

Wakati unajenga timu, wengi waliamini Yanga ni ile ile ya kina Sarpong, tunakuja kushtuka Yanga unatimu bora sana. Kuja kuamka usingizini ni too late.
 
Peter Banda alikua na Umri gani na si alitoka ulaya Team iliyoifunga Madrid UEFA tena Bernabeu?
Peter Banda japo sio mzuri kwa ubora wa Jean, ila hakuwa mbaya yule mtoto.

Injury, Injury ndio mchawi mkubwa wa viwango vya wachezaji wengi.
 
Tunaomba takwimu zao wote kuanzia Aziz ki alivyokua Mvp na pacome pia ndio umalizie na huyo ili tu ujue ka yaliyomo yamo?
Takwimu pekee haziwezi kukupa picha kamili kuhusu ubora wa mchezaji, japo zina nafasi yake katika kutambua ubora wa mchezaji.

Ndio maana Mascout wanazunguka katika mechi, ili kujua uhalisia wa mchezaji. Nenda kaangalie baadhi ya mechi zake na ukijumlisha kwa takwimu basi utakuja kukubaliana na kupinga na hiki kilichosemwa.
 
Tuwape muda simba sasa hivi bado wanakusanya hatua ya pili wanatakiwa kuelewana hii ndio kazi kubwa ya kocha.
 
Hiyo nafasi ya takwimu ndio naitaka Mimi maana ndio rahisi kujua kuliko kuzunguuka viwanjani kama scout
 
Umeanza kufuatilia mpira lini
 
Kramo alikuwa ni moja ya Wachezaji bora sana. Ila narudi tena, kama nilivyosema hapo awali kwamba; Injury ndio mchawi mkubwa wa vipaji vya wachezaji.
Jujuumkuuu achakabisaa
 
Haya sasa waje waliokuwa wanabeza huu usajili
 
Haya sasa waje waliokuwa wanabeza huu usajili
Vs mechi ya Tabora iliyozuiwa kuchezeshwa wachezaji wa kigeni na Fountain gate iliyozuiwa kutumia wachezaji wa kigeni. Mna haraka sana ya kuhitimisha wakati muda bado sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…