Namshukuru Mungu leo tar 9/5 nimetimiza miaka 33 kamili wengi wamepotea kabla hawajafika huku na walikua na ndoto nyingi,wote ambao tumefika huku tukiwa na afya njema tuungane kumshukuru Mungu .Pia furaha yangu kubwa nimetimiza kigezo anachokitaka inna morata kwani ndio ilikua kigezo pekee ninachomiss cha miaka 33 minimum kwa hiyo baada ya hii thread naenda pm nikiwa kifua mbele
Duuh! Hongera sana!
Nasikitika tu Mwalim Nyerere mwanzilishi wa Taifa letu na sera zake za ujamaa na Azimio la Arusha na mwanzo wake huujui,
Elimu bure ya kutoka shule ya msingi mpaka chuo kikuu huijui, mavazi ya Chu in lai huyajui, kupinduliwa kwa Obote na Idi Amin Dada hukushuhudiavita, Kifo cha Jomo Kenyatta na Harambee ya wana Kenya hukushuhudia, Vita vya Kagera against Idi Amin Dada wa Uganda huijui, Ndege za Mc Donnell Douglas DC 9 na Vickers VC 10 za East African Community
نتيجة بحث Google عن الصور حول https://cdn.jetphotos.com/full/2/29327_1084793371.jpg na huo umoja kuvunjika huujui nahujaziona, kujengwa kwa Tazara na barabara ya Tanzania na Zambia na wachina hukushuhudia, mapinduzi ya watanzania walio taka kumpindua Nyerere hukushuhudia na Nyerere kuwasamehe wote, kujiuzuru kwa Wwalim Nyerere kuwa Rais na kumkabidhi madaraka ya urais Ali Hassan Mwinyi hukushuhudia, mgogoro kati ya Ali Hassan Mwinyi na Mwalim Nyerere kuhusu majukumu ya tutawala kati yao (Mwinyi Rais na Nyerere mwenyekiti wa CCM) hujayashuhudia. Kijana, Duuh! Ume yakosa mengi lakini!
Na watu kama mimi kwa mfano nimepitia Tanu Youthleage, nimekwenda kusoma Ulaya, nina Masters, nimeoa mzungu, nina watoto wawili mmoja wa kike na mwingine wa kiume ambao wote wako Ulaya mmoja UK na mwingine Deutschland, nimefanya kazi Ulaya na kuwatumikia wazungu, na sasa naishi kwetu Bongo na kulitumikia Taiafa letu kwa mshahara mdogo bila malalamikio nitashukuru vipi?
Nilikuwa tu nakusii hizo hoja nyingine nafuu uziache akilini kwako, kwani hazina mantiki yoyote katika jukwa hili!