Ahsante Ndugai, tutakuelewa baadae baada ya mnada

Ahsante Ndugai, tutakuelewa baadae baada ya mnada

HANGAYA THE CHIEF

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2021
Posts
330
Reaction score
962
Napongeza kauli ya Mh. Spika, imetoka sehemu nyeti sana na kwa mtu asiyetegemewa kusema aliyoyasema, lakini ameyasema mimi kwangu ni ushujaa na upendo kama yamesemwa katika jicho pana la tahadhari ambayo katika nafasi anajua na kuyaona zaidi kuliko sisi wapiga zumari.

Kwa kifupi zimesemwa na mtu aliyepo jikoni. Swali letu lisingekuwa kukosoa, pengine ningepata nafasi ningependa kujua kwa nini sasa? au kaona nini katika mikopo inayochukuliwa sasa?

Muhimu kujua kuwa ibara ya 4 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, inatabainisha ukuu wa uongozi wa mihimili mitatu, hivyo kauli yeyote ya rais, jaji mkuu, au spika wa bunge si za kubezwa wala kuziwekea siasa, na hasa zinapogusa maslai mapana ya taifa letu. nachelea kukubali kuwa spika alipitiwa kuongea kuwa kuna siku nchi itapigwa mnada kwa sababu ya kutembeza bakuli.

Kwani kitaalamu na kwa uelewa mdogo wa sera za fedha na zaidi sana ukusanyaji wa mapato. kwangu mimi ningesema Spika yuko sahihi kabisa, kimsingi lazima kuwe na uwino wa mapato na matumizi, na tukiamua kukopa mara nyingi ni last option for strategic plan.

Mfano tozo na pesa za mkopo wa covid-19 ambazo kwake alitolea mfano, kuwa tumeshangilia na kupigia makofi nchi zima, ambazo zinakwenda kutekeleza kitu kile kile, kwa maana nyinge alikuwa anatueleza nini logic ya kuwa na tozo, na kwenda kukopa kutekeleza kile ambacho tozo zinafanya?

Binafsi kauli yake, isichukuliwe kama anampinga mama, bali kama tahadhali juu ya wataalam wetu wanaoshughulikia mambo ya fedha na kuratibu mikopo, bado tuna sehemu kubwa haijatekelezwa katika ukusanyaji wa mapato, tuna madini, na rasilimali nyingi ambazo kwayo tunaweza kujenga nchi yetu.

Kwangu mimi, mate ni mate hata kama yakitemwa na maskini au tajiri. Spika kaongea ukweli mchungu, ni kama baniani mbaya ila kiatu chake ni dawa. tunapashwa kuupokea na kuufanyia kazi.
 
Aseeeee ndugai ana nguvu saana aseee

Yani kila anaesimama anashambulia hoja ya ndugai
 
Nawaza sisi tutaenda wapi? Au ndo tutakuwa cheap labours kama wa southafrica na wakenya
 
Wacha yamkutee tu kazid jeuli
 
Back
Top Bottom