sio kama zanzibar hakuna watu wenye ujuzi, lakini tatizo la ZNZ siasa mbele, mara nyingi wanachaguliwa watu kwa utashi wa kisiasa wewe tizama baraza letu la wawakilishi (CCM) aibu tupu wawakilishi wanashindwa hata kujieleza , tunadhalilika sana ZNZ kwa upuuzi huu wa kila kitu siasa mbele.
Naweza kumkingia kifua Bw. Juma hapo. Wewe hukuwepo katika hiyo semina, naamini ungemuelewa vizuri kutokana na upeo wako, na Wawakilishi waliokuwa wakimsikiliza najuwa wamemuelewa vizuri. Tatizo la sisi kuelewa vibaya limechangiwa na uandishi mbovu wa Mwandishi aliyeandika habari hiyo. Ni mwanagenzi na amefanya "quotations" visivyo hivyo amepotosha badala ya kupasha habari. Taaluma hiyo Mzee -imekwenda kombo hapo.
Huyu kiongozi wa upinzani ana maana gani anaposema hivi? ana ushahidi ambapo wazanzibari wameshughulikiwa kwa sababu tu ni wazanzabari? Huyu ana tofauti gani na yule aliyedai watu wa Monduli wanaonewa? Nimesoma na kufanya kazi na wazanzibari na sijaona mahali ambapo wamenyanyaswa kutokana na uzanzibari. Wenzetu walikuwa hata wakimaliza kidatu cha sita hawahusiki na JKT na hakuna aliyelalamika. huyu bwana kwa sababu huko wana hisia za kukomoana kati ya waunguja na wapemba anataka kutuletea sisi? Kwa vile avaae kiatu ndiye anayejua kinapombana, atutajie majina ya hao waliopatwa na hiyo dhoruba ili wote tutambue kuwa serikali ya Muungano ni ya kibaguzi. Kama hawezi, anyamaze na awaombe msamaha wale wanaowaita machogo wote! Ni vijineno kama hivi vya uchonganishi ndiyo mwanzo wa matatizo mengi katika jamii zetu.
Epa,richmond,makaa Ya Mawe Kiwira Na Sasa Chenge Na Rada!!!! Yote Hayo Hakuna Linaloendelea Katika Nchi Hii,kisha Mnaanza Kuangalia Nafsi Za Ajira Zanzibar Ndani Ya Bot,mpika Chai Ndio Nini,mlinzi Ndio Nini!!! Zote Kazi,it Na Mambo Mengine Zote Kazi Ndani Ya Bot.je Nawauliza Wazanzibar Wenzangu,sector Ya Utalii Mbona Wameasha Wageni Wakitawala Kila Hotel Bila Kujua Kama Uchumi Wao Unapotea Na Watu Wengi Kukosa Ajira!!!! Tuangalia Kwanza Utalii Sisi Ndio Utatulipa!!!!
Mheshimkiwa Fundi. Upande huo Bwana jazba mbele . Wao katika kila kitu jazba zinatawala. Kuna watu wazuri na wasomi, lakini wote wana ka -mdudu jazba .Huharibu mambo tu.Huyu kiongozi wa upinzani ana maana gani anaposema hivi? ana ushahidi ambapo wazanzibari wameshughulikiwa kwa sababu tu ni wazanzabari? Huyu ana tofauti gani na yule aliyedai watu wa Monduli wanaonewa? Nimesoma na kufanya kazi na wazanzibari na sijaona mahali ambapo wamenyanyaswa kutokana na uzanzibari. Wenzetu walikuwa hata wakimaliza kidatu cha sita hawahusiki na JKT na hakuna aliyelalamika. huyu bwana kwa sababu huko wana hisia za kukomoana kati ya waunguja na wapemba anataka kutuletea sisi? Kwa vile avaae kiatu ndiye anayejua kinapombana, atutajie majina ya hao waliopatwa na hiyo dhoruba ili wote tutambue kuwa serikali ya Muungano ni ya kibaguzi. Kama hawezi, anyamaze na awaombe msamaha wale wanaowaita machogo wote! Ni vijineno kama hivi vya uchonganishi ndiyo mwanzo wa matatizo mengi katika jamii zetu.
Akijibu madai hayo, Reli alisema nafasi ambazo Wazanzibari wanaweza kupewa zisizokuwa na ushindani wa sifa ni zile za kupika chai, ulinzi na udereva, lakini nafasi nyengine zote za kitaalamu zinatakiwa kuombwa na watu wenye sifa na hakuna nafasi maalumu zilizotengwa kwa ajili ya Wazanzibari.
"Waheshimiwa wajumbe nafasi za ajira ya kupika chai, ulinzi na udereva hizi Wazanzibari wanaweza kuzifanya na ni zao hatuna sababu ya kumchukua mpika chai au mlinzi ama dereva kutoka Tanzania Bara, lakini zile za kitaalamu kama uhasibu, IT na nyinginezo, hizo ni lazima watu waombe na kushindaniwa na Watanzania wote wenye sifa," alisema Naibu Gavana.
Majibu hayo yaliwachukiza karibu wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi ambao wasisitiza kwamba Zanzibar wapo watu wenye sifa ambao wanaweza kufanya kazi za kitaalamu.
Hata hivyo, mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi wa Baraza la Wawakilishi, Salmin Awadh Salmin alikiri kuwa ni kweli vijana wengi wa Zanzibar hawana sifa za kuwawezesha kuajiriwa katika kazi za kitaalamu BoT.