Ahsante sana mwanakijiji wewe ni mzalendo wa kweli

Mtz-halisi

Member
Joined
Nov 28, 2009
Posts
47
Reaction score
20
Kwa niaba ya wanachama wa CHADEMA twasema ahsante. Uchambuzi wako ulikuwa ni mzuri na wa Busara kubwa, ushauli wa kujenga. Najua imepita siku nyingi toka uandike ushauli wako; Viongozi wa CHADEMA wamesikia na watafanyia kazi. ila sijui kama ndugu Zitto alisoma na kuuelewa.

Tuzidi kuomba juu ya nchi yetu na juu ya wanasiasa wetu. haya unayo yaona sasa ni majibu ya Mungu aliye hai, Muumba Mbingu na nchi. Yeye aliweka mambo hazarani mapema sana na siyo mwanadamu awaye yote.

Nawatakia wananchi Merry Christmas and Happy new year.

Tunaomba hekima ya Mungu juu ya viongozi wetu; Tunawaombea vijana nidhamu na utii, tunaomba juu ya Katiba mpya na pia tunaomba juu wananchi wote wa Tanzania.
 
Uzalendo ni kwa Taifa tu
kusaliti Taifa kwa ajili ya chama sio uzalendo....ni usaliti

Daa!, Kila nikifuatilia comments zako katika siasa uwa unaziweka kimafumbo.

Leo ningeomba ufafanuzi Juu ya hii comment.
 
Mwanakijiji anapaswa kujiuliza
je katika harakati zake za kuitoa CCM na kuiweka CHADEMA madarakani
hawahi kuvuka mstari wa kusaliti Taifa kwa ajili ya CHADEMA?
wazungu wanaita ku justify the means to an end
 
Kwa niaba ya wanachama wa CHADEMA twasema ahsante. Uchambuzi wako ulikuwa ni mzuri na wa Busara kubwa, ushauli wa kujenga. Najua imepita siku nyingi toka uandike ushauli wako; Viongozi wa CHADEMA wamesikia na watafanyia kazi. ila sijui kama ndugu Zitto alisoma na kuuelewa.

Tuzidi kuomba juu ya nchi yetu na juu ya wanasiasa wetu. haya unayo yaona sasa ni majibu ya Mungu aliye hai, Muumba Mbingu na nchi. Yeye aliweka mambo hazarani mapema sana na siyo mwanadamu awaye yote.

Nawatakia wananchi Merry Christmas and Happy new year.

Tunaomba hekima ya Mungu juu ya viongozi wetu; Tunawaombea vijana nidhamu na utii, tunaomba juu ya Katiba mpya na pia tunaomba juu wananchi wote wa Tanzania.

Kwa kauli kama hizi lazima Mchungaji Msigwa na Padre Slaa watashinda dhidi ya bwana Zitto Zuberi Kabwe.

Btw, sio ushauli ni ushauri mtumishi wa bwana.
 
Mwanakijiji anapaswa kujiuliza
je katika harakati zake za kuitoa CCM na kuiweka CHADEMA madarakani
hawahi kuvuka mstari wa kusaliti Taifa kwa ajili ya CHADEMA?
wazungu wanaita ku justify the means to an end

Kama umewahi kunisoma vizuri mimi si muumini wa hii nadharia ya "utaifa kwanza"..... ina makosa mengi ya kifaslafa.
 
Uzalendo ni kwa Taifa tu
kusaliti Taifa kwa ajili ya chama sio uzalendo....ni usaliti

Mkuu kwenye upande huo naweza kusema nchi yetu ni jamhuri ya ndizi, mpaka sasa bado wanasiasa wengine wanaonesha kujali zaidi maslahi ya vyama vyao na ya kwao binafsi. Kweli ni usaliti kuziweka interests zetu binafsi na za vyama vyetu mbele kuliko nchi yetu. Tusipo badilisha hilo naweza kusema tutaendelea kupiga mark time
 
Mwanakijiji anapaswa kujiuliza
je katika harakati zake za kuitoa CCM na kuiweka CHADEMA madarakani
hawahi kuvuka mstari wa kusaliti Taifa kwa ajili ya CHADEMA?
wazungu wanaita ku justify the means to an end

Kama umewahi kujisoma vizuri mimi si muumini wa hii nadharia ya "utaifa kwanza"..... ina makosa mengi ya kifaslafa.

Kuna watu wanatumia shortcut sana kutofautisha nadharia hizo za "utaifa kwanza" na "chama kwanza."

Ingawa ni kweli kuwa utaifa ndio jambo la muhimu kuliko ubinafasi, lakini unapotaka kutetea "utaifa kwanza" ni lazima kwanza upige vita serikali iliyoko madarakani iwapo yenyewe haitetei utaifa. Wataalamu (siyo mimi) wanafananisha taifa na hardware, serikali na Kernel, halafu sisi wanachi ndiyo applications za hiyo system. Hata ukiwa na application nzuri kiasi gani, kama kernel ni mbovu basi hardware yako haitafanya vizuri, so kutetea hardware ni lazima pia uangalia ile kernel inaiyoendesha, na hapo ndipo chama kinapoingia kwenye mzunguko. Ukihasi chama chako ili utetea taifa wakati ni wazi kuwa chama kinachoendesha serikali kina mtazamo tofauti huwezi kufika popote hata kama kelele zako zinasikika na kupendwa na watu wengi.
 
Kweli kabisa; hakuna nchi duniani inayoongozwa na "utaifa kwanza" nje ya vyama vya siasa isipokuwa mahali ambapo kumetokea mapinduzi ya kijeshi. Lakini pia suala la 'utaifa kwanza' halina sera au ilani - unapotaka 'utaifa kwanza' unataka kutekeleza sera za nani na zinaundwa na nani na watu hao wanasimamiwa na nani?
 
Hivi watu wanatifautishaje taifa na chama halali cha siasa? hivi ukifanya siasa ndani ya chama huwezi kuwa na faida kwa taifa? Sera za kifisadi hizi ni kutia watu ujinga tuu... Hongera Mzee Mwanakijiji
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana comrade popote pale ulipo Mungu akupe afya njema ccm wapo intensive care unit.
 
Kweli kabisa; hakuna nchi duniani inayoongozwa na "utaifa kwanza" nje ya vyama vya siasa isipokuwa mahali ambapo kumetokea mapinduzi ya kijeshi. Lakini pia suala la 'utaifa kwanza' halina sera au ilani - unapotaka 'utaifa kwanza' unataka kutekeleza sera za nani na zinaundwa na nani na watu hao wanasimamiwa na nani?
Maslahi binafsi hujificha katika kivuli cha maslahi ya taifa kwa kuwa taifa huwa halina vikao vya kujadili na kuhoji ukweli wa kinachoitwa maslahi yake. Lakini chama ni mkusanyiko/muungano wa watu wenye muono,lengo,mbinu na imani/itikadi unaofanana katika kushika mamlaka au kushinda taji fulani. Watu hawa huweka malengo na mbinu zao katika kanuni ambazo huitwa katiba. Ili chama kifikie malengo lazima iwepo nidhamu baina ya watu walioungana kwa lengo moja, kukosekana kwa nidhamu ni sawa na kushindwa hata kabla ya mashindano kuanza.
 
Kuna watu wanatumia shortcut sana kutofautisha nadharia hizo za "utaifa kwanza" na "chama kwanza."

Ingawa ni kweli kuwa utaifa ndio jambo la muhimu kuliko ubinafasi, lakini unapotaka kutetea "utaifa kwanza" ni lazima kwanza upige vita serikali iliyoko madarakani iwapo yenyewe haitetei utaifa. Wataalamu (siyo mimi) wanafananisha taifa na hardware, serikali na Kernel, halafu sisi wanachi ndiyo applications za hiyo system. Hata ukiwa na application nzuri kiasi gani, kama kernel ni mbovu basi hardware yako haitafanya vizuri, so kutetea hardware ni lazima pia uangalia ile kernel inaiyoendesha, na hapo ndipo chama kinapoingia kwenye mzunguko. Ukihasi chama chako ili utetea taifa wakati ni wazi kuwa chama kinachoendesha serikali kina mtazamo tofauti huwezi kufika popote hata kama kelele zako zinasikika na kupendwa na watu wengi.

Na hapa ndipo ZZK anapokosea kwa kuanza kusema...nita....nime...nili....UMIMI
 
poor and un realistic theories

mapinduzi yote na mabadiliko yote dunia hii yameanzishwa na mtu mmoja na sio taasisi

taasisi iko kubeba ndoto za mtu

HAKUNA TATIZO NA hizo sentensi, woga wako na wivu wako

watoto wa mbowe bana,
 
mwanakijiji unadanganya watu, viti maalumu chadema utapata usihofu
 
poor and un realistic theories

mapinduzi yote na mabadiliko yote dunia hii yameanzishwa na mtu mmoja na sio taasisi

taasisi iko kubeba ndoto za mtu

HAKUNA TATIZO NA hizo sentensi, woga wako na wivu wako

watoto wa mbowe bana,

Sasa do you see any spirit ya utaasisi kwenye kauli na matendo ya ZZK, ww ndio mwenye theories za ajabu, wazo la mapinduzi ndio linaweza anzishwa na mtu mmoja lakini implementation lazima ihusishe watu. Hii sio kwenye politics tu, hata katika science....There has never existed a one man army that fought a battle and won,,,,,

Mdanganye tu huyo jamaa, tutaona. By the way kwa nini niwe na wivu nae...Nlitaka kumsaidia kwa ushauri wangu, unless haipendi CDM anayohubiri mdomoni kuipenda...
 
Eti "watoto wa Mbowe bana"
Kwani huyo unayemtetea ni mtoto wa nani?, bila juhudi binafsi za Mbowe, huyo Zitto ungemsikia wapi?
Muulize huyo Zitto ametolewa wapi na Mbowe, na, halafu, kama kitu hujui uliza.
poor and un realistic theories

mapinduzi yote na mabadiliko yote dunia hii yameanzishwa na mtu mmoja na sio taasisi

taasisi iko kubeba ndoto za mtu

HAKUNA TATIZO NA hizo sentensi, woga wako na wivu wako

watoto wa mbowe bana,
 
Wakuu mnatoa elimu nzuri sana ingawa sijui wangapi wanaipata. Kuna ubabaishaji umeenezwa sana na viongozi hapa nchini. Mara utasikia kauli kama "tuwe na uzalendo"; "katika suala hili, tunaangalia maslahi ya taifa tu na si itikadi za vyama"; "utaifa kwanza, vyama baadaye"; "tusiingize siasa kwenye mambo muhimu ya taifa"! Mpaka mtu unawaza kama siasa na vyama havina maana kwa nini tusiachane navyo kabisa?

Tatizo wengi hata maana ya neno "ITIKADI" hawaijui; wanafikiri ni tofauti ya majina ya vyama. Na wajanja wanaotaka kutupoteza kwa maslahi yao ya kifisadi baada ya kushindwa kutoa SIASA SAFI na UONGOZI BORA, wamekuja na gia ya kutudanganya kwamba siasa (itikadi) na vyama vya siasa havina nafasi katika maendeleo na ustawi wa taifa bali "uzalendo" na ndugu yake "utaifa kwanza" kama vile tunu hizo zinakuja kwa bla bla bila dira na uongozi sahihi.

Wachina juzi tu wamefikisha chombo kwenye mwezi kwa sababu wana chama cha siasa (hata kama ndicho pekee tu) chenye siasa (itikadi) inayoelekeza kwenye maendeleo makubwa ya kiteknolojia na uongozi uliojizatiti kutekeleza azma hiyo - kuanzia kwenye kujenga uwezo wa kitaaluma wa watu wake hadi kuwawezesha kufanya mambo makubwa kama hayo tena kwa kutumia lugha yao. NA kwenye hilo, hawachekei mtu anayejaribu kuwahamisha kwenye lengo.
 
Mkuu kwenye upande huo naweza kusema nchi yetu ni jamhuri ya ndizi, mpaka sasa bado wanasiasa wengine wanaonesha kujali zaidi maslahi ya vyama vyao na ya kwao binafsi. Kweli ni usaliti kuziweka interests zetu binafsi na za vyama vyetu mbele kuliko nchi yetu. Tusipo badilisha hilo naweza kusema tutaendelea kupiga mark time

Chama makini (credible) hakiwezi kuwa na maslahi tofauti na ya taifa lake; hili lipo kwa chama mamluki tu. Mtu binafsi ni habari nyingine; anaweza kujificha katika kivuli cha unafiki kufanikisha maslahi yake yasiyo na tija kwa taifa - hata akiwa ndani ya chama makini.
 
"There has never existed a one man army that fought a battle and won". Nimeipenda sana hii na ZZK mwisho wa siku Ujanja wake utakwisha; Lamwai, Nsanzugwako, Hiza Tambe na wengine wengi ni mifano tosha.Ni swala la muda tu maana huyu Kijana anaendelea kupiga ngumi zake ukutani.
 
Back
Top Bottom