Mnyika point nzuri sana; na tumekuwa katika mazungumzo na CPJ na ninatumaini Polisi watatoa tamko lao mapema kabla hatua za kisheria dhidi yao hazijachukuliwa. Wasidhani kumwachilia mtu kimya kimya kunamaliza hoja.
a. Kitendo cha kumkatama mtu na kumhoji kwa masaa karibu ishirini bila warrant au amri halali ni kitendo cha kiunyanyasaji na uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu.
b. Kitendo cha wao kuwahusisha vijana hawa na mtandao wa ughaidi siyo tu kumewachafulia majina yao bali pia kumesababisha wakose nafasi nyingi za kuaminiwa na hivyo kufanya maisha yao kuwa magumu pasipo ulazima wowote.
c. Kitendo cha Jeshi la Polisi kuchukua mali za vijana hawa kuziangalia, na kuzifanyia uchunguzi pasipo amri yoyote ya wao kufanya hivyo ni kinyume cha Katiba na kinaangilia mawasiliano ya mtu na kuvunja sheria.
d. Kitendo cha Polisi kuwashikilia vijana hawa kilisababisha hali ya wasiwasi, hofu, maumivu, hofu, woga, usumbufu kwa ndugu jamaa na marafiki; kilisababisha nyumba ya mmoja wao kuingiliwa na kuibwa vitu baada ya kujulikana hayupo nyumbani hasara ya karibu shilingi milioni 50!
e. Mmoja wao alikuwa anafuga kambwa kadogo kadogo ambako kalitoweka hadi leo hakajapatikana na inadaiwa kalipigwa mawe na mzoga wake kukutwa kawe karibu na "Stendi ya Basi". Mnyama huyo na mlinzi wa nyumbani alifanyiwa hivyo baada ya Polisi kumshikilia mwenyewe. Uchungu wa kufiwa na kambwa hako kakali umesababisha huzuni na uchungu ambao unakadiriwa kufikia shilingi milioni 10.
Baada ya kuangalia hayo yote na kwa vile jeshi la Polisi na serikali hawajaomba radhi na kusema kuwasafisha vijana hawa hadharani na kuahidi kutokuwanyanyasa tena kunasabisha a pending lawsuit ambapo madai ya karibu shilingi milioni 70 ya madhara (damages) yatadaiwa na shilingi milioni 200 ya adhabu (punitive).
Ila wakiamua kuomba radhi mapema wiki ijayo, we'll rethink some of our options na kujaribu kusettle for "undisclosed amount".