Ahsanteni jirani zetu Kenya mmetufaa sana wakati huu

Ahsanteni jirani zetu Kenya mmetufaa sana wakati huu

mmteule

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
6,035
Reaction score
15,080
Muungwana siku zote lazima ushukuru kwa wema unaotendewa na kusema Ahsante. Ndugu zetu na jirani Zetu Wakenya, hakika mmeonyesha kile wahenga walituusia "RAFIKI WA KWELI NI YULE AKUFAAYE WAKATI WA DHIKI".

Wakati wa Msiba na Maombolezo ya Rais wetu wa JMT Mhe.Magufuli. Mmeonyesha kuguswa na Masikitiko kwa maneno ya Faraja kuanzia kwenye Ikulu ya Mhe. Kenyata mpaka kwenye mitaa ya Kibera.

Mmeshirikiana nasi mpaka kwenye Mitandao ya Kijamii kupambana na Jumuia za Kimataifa zinazoizodoa Tanzania kwa kusimama nasi kama Jirani zenu wa Damu.

Kwa sisi waungwana hatuna cha kuwapa zaidi ya Kusema Ahsanteni sana jirani zetu Wakenya, mmetuonyesha kuwa hizi Ligi za Maneno baina yetu na nyie ni utani tu wa mitandaoni

Mhe.Kenyata kaka yangu popote ulipo. Hakika umejijenga kwenye mioyo yetu sisi Watanzania kuanzia jinsi ulivyoomboleza nasi, ulivyopeperusha bendera nusu mlingoti kwa siku kadhaa. Kwenye jumuia ya Kiiislam kwa kuitii Adhana na kutambua hili BAKWATA tayari wametambua weledi wako.

Jirani zetu mmetufaa, mmetufariji, mmesimama nasi na Hatuna cha kusema zaidi ya MWABHEJA SANA WAKENYA.

IMG-20210325-WA0067.jpg

IMG-20210325-WA0068.jpg

IMG-20210325-WA0069.jpg

IMG-20210325-WA0070.jpg

IMG-20210325-WA0071.jpg

IMG-20210325-WA0072.jpg
 
Waafrika yatubidi kushikamana. Mwafrika jirani ni wa kushikana naye zaidi kuliko mwingine yeyote.

Tusikubali kwa namna yoyote ile kumfanya jirani yetu kuwa adui. Kwa kuangalia historia na mazingira yetu, Kenya ni ratiki yetu no. 1, kisha Uganda, Malawi, halafu Zambia, Msumbiji, Rwanda, Burundi na DRC.

Katika hawa, hatutakiwi kumpata adui.

Kutofautiana kupo, ndiyo maana hata watoto wanaofuatana, kuna wakati mpaka hupigana, lakini mioyoni mwao wanajitambua kuwa wao ni wa karibu zaidi kuliko mwingine yeyote.

Tunatakiwa kuwa na uhusiano mzuri na kila Taifa lakini uhusiano mzuri na nchi jirani ni kipaumbele cha kwanza.
 
Hakika Mkuu.
 
Kuna vitoto vya Jirani hapa ni Mapacha, muda wote vinagombana na kupigana. Lakini mama yao akishika fimbo akamchapa say Dotto utashangaa jinsi Kulwa anakuwa mkali na kupambana na Mama yao amwache Mdogo wake. Akishindwa kabisa anamwambia mamake basi nichape na Mimi kama umemchapa huyo.

Ugomvi na mama ukiisha wenyewe Kwa wenyewe wanaendelea Navy ugomvi wao.

Naona Wakenya wamedhihirisha kuwa Kenya na Tz ni watoto Mapacha. Daima hawapatani, lakini mtu baki ukijifanya kuingilia kati ukagusa mmoja, wote wanakuchangia kukutia adabu..

Wakishamalizana na Wewe Bifu lao linaendelea.
 
Back
Top Bottom