Waafrika yatubidi kushikamana. Mwafrika jirani ni wa kushikana naye zaidi kuliko mwingine yeyote.
Tusikubali kwa namna yoyote ile kumfanya jirani yetu kuwa adui. Kwa kuangalia historia na mazingira yetu, Kenya ni ratiki yetu no. 1, kisha Uganda, Malawi, halafu Zambia, Msumbiji, Rwanda, Burundi na DRC.
Katika hawa, hatutakiwi kumpata adui.
Kutofautiana kupo, ndiyo maana hata watoto wanaofuatana, kuna wakati mpaka hupigana, lakini mioyoni mwao wanajitambua kuwa wao ni wa karibu zaidi kuliko mwingine yeyote.
Tunatakiwa kuwa na uhusiano mzuri na kila Taifa lakini uhusiano mzuri na nchi jirani ni kipaumbele cha kwanza.