Ahsanteni Mabasi ya Mwendokasi

Rohombaya

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
13,067
Reaction score
10,393
Dah... leo zilinitembelea nikaamua kwenda kula maisha...juakali nikaona isiwe tabu ngoja nipande mwendokasi kutoka Fire hadi Kisutu....mbona pesa ninayo....
Kituo cha Fire kina urefu wa karibu mita 180.
Nilipoingia kituoni nikaona basi la Kivukoni linaingia kwa kasi nami nikatoka mbio nalikimbiza kuanzia mwanzo wa kituo hadi mwisho nalikimbiza bahati mbaya nikazidiwa ile nafika ndiyo milango inafungwa....likaniacha.
Kuangalia nikaona jingine limesimama mwanzo wa kituo ... nikatoka nduki tena.. lakini likaniacha....Ikanibidi nitumie akili ya kuzaliwa...nikavua kandambili kisha nikakasimama katikati ya kituo huku nikipasha misuli moto ili likitokea upande wowote niliwahi...ndiyo nikaweza kupanda...
Sikuona maelekezo yoyote ya abiria anayeenda wapi asimame wapi... Labda kama yapo yalioandikwa kiingreza...mita 180 si kidogo
Ila mmeniweza sana kunikimbiza mita 650 kwa shuruti.......πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜Ž
 
Teh teh hii story imenikumbusha ile karamu ya fisi, aliends kwenye sherehe ya kwanza akaukta chakula bado, akarudi kwenye ya pili akakuta chakula kimeshaisha...
 
Hahaha Upo vyema kutupotezea Kidogo mawazo
 
Yaani nimecheka saaanaaa!
Umenikumbusha majuzi nilishikwa na hasira sana nikiwa hapo kituoni Faya!
Nilikuwa nasubiri basi la Moroko, nililisubiri zaidi ya nusu saa! Kwanza yalipita bila kusimama na likisimama si pale walipo abiria!
Bahati nzuri alitokea jamaa ana beji ya UDART nilianza kumueleza hivyo vituko vyao......alicheka tu!
Nikamuuliza ni kwanini wasiweke vibao kuelekeza basi la wapi linasimama kushusha au kupakia kama ilivyo Moroko ama Kivukoni?
Alielewa na akaahidi kulifikisha kunako!
Kwa kweli ni kero sana!
Pole sana ndugu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…