Rohombaya
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 13,067
- 10,393
Dah... leo zilinitembelea nikaamua kwenda kula maisha...juakali nikaona isiwe tabu ngoja nipande mwendokasi kutoka Fire hadi Kisutu....mbona pesa ninayo....
Kituo cha Fire kina urefu wa karibu mita 180.
Nilipoingia kituoni nikaona basi la Kivukoni linaingia kwa kasi nami nikatoka mbio nalikimbiza kuanzia mwanzo wa kituo hadi mwisho nalikimbiza bahati mbaya nikazidiwa ile nafika ndiyo milango inafungwa....likaniacha.
Kuangalia nikaona jingine limesimama mwanzo wa kituo ... nikatoka nduki tena.. lakini likaniacha....Ikanibidi nitumie akili ya kuzaliwa...nikavua kandambili kisha nikakasimama katikati ya kituo huku nikipasha misuli moto ili likitokea upande wowote niliwahi...ndiyo nikaweza kupanda...
Sikuona maelekezo yoyote ya abiria anayeenda wapi asimame wapi... Labda kama yapo yalioandikwa kiingreza...mita 180 si kidogo
Ila mmeniweza sana kunikimbiza mita 650 kwa shuruti.......😀😀😀😎