Wakuu poleni na kazi. Niende kwenye hoja.
Kwa saa ishirini na nne zilizopita kumekuwa na sauti (audio) mtandaoni ikidaiwa ni ya Mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Shabiby akiwaelekeza watu wake wamkamate na kwenda kumlawiti mwananchi aliyempigia simu kumuuliza habari za maendeleo ya jimboni kwake (Gairo).
Audio hiyo imerushwa na wanaharakati wawili wa kike ambao wanaishi nje ya nchi huku ikizua taharuki kuhusu usahihi wa sauti na ukweli wa maagizo hayo ya mbunge kwa mwananchi wake.
KWA MUJIBU WA CHANZO, SAUTI INA MWAKA MMOJA SASA!
Sasa isivyokuwa bahati, mbunge huyo alipotafutwa ili kusikia chochote kutoka kwake hakupatikana mara moja.
Lakini kwa mujibu wa vyanzo viwili vya ukakika ni kwamba, sauti inayodaiwa ni ya mbunge Shabiby imeundwa na Akili Unde (Artificial Intelligent) kwa lengo la kumchafua kimkakati.
Pili; sauti hiyo ilitengenezwa na mtu mmoja wakati wa Kura za Maoni ndani ya CCM, Julai mwaka 2025 ili kumwingiza mbunge huyo katika skendo.
"Hii Audio alitengeneza jamaa mmoja wakati wa Kura za Maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi kwenye kinyang'anyiro cha ubunge. Kwa hiyo ni sauti yenye mwaka mmoja sasa tangu itengenezwe," kilisema chanzo.
"Mheshimiwa Shabiby huwa anapigiwa simu na wapiga kura wake wengi tu. Tena kila siku. Wengine huwa anawaita wakutane ana kwa ana. Wengine wanamalizana kwenye simu. Lakini hakuna aliyewahi kumtisha kwa namna yoyote ile.
Chanzo hicho kikaongeza: "Hivi mtu unaweza kutumia akili kujiuliza swali hili. Ni kweli mbunge anaweza kuagiza mpiga kura wake akamatwe na kulawitiwa, eti kwa sababu tu ameuliza swali la kuhusu maendeleo ya jimboni kwake? Inawezekana kweli?"
"Mbona wabunge wengi wanapozungumza bungeni tunawaona wakisema wananchi wao wanawauliza kuhusu maendeleo ya barabara. Kuhusu maji.
Kuhusu ujenzi wa zahanati au shule. Kama ni makosa si wangekuwa wanakamatwa na kulawitiwa au kuadhibiwa kwa wingi?" Kilihoji chanzo hicho kikimkosoa mtu aliyedai ndiye aliyeitengeneza sauti hiyo.
MASWALI YA KUSHANGAZA KUHUSU ALIYEPIGA SIMU!
Aidha, chanzo hicho kikasema, wanaharakati hao wameandika kuwa, mwananchi huyo anaishi kwa hofu kwa sasa.
Akahoji: "Kama ni kweli na anamjua Shabiby na namba yake ya simu anayo, maana alimpigia, kwa nini asiende polisi kuripoti kitisho hicho ili asiishi kwa hofu tangu mwaka jana mwezi wa saba?"
MUUNGANISHA SAUTI SIYO MPINZANI
Chanzo cha pili kilisema kuwa, kinachoshangaza ni mtu aliyeunda sauti hiyo na kuunganisha na sauti nyingine ya mbunge huyo kwamba, siyo wa kutoka upinzani.
"Adui wa mhehsimiwa siyo mpinzani. Ni mtu anayefahamika. Ndiyo maana ukifuatilia watoa maoni wengi wanamtetea mheshimiwa Shabiby kwa sababu adhabu inayodaiwa alitakiwa apewe mtu huyo haifanani ya 'kosa' la swali alilouliza," kilisema chanzo hicho cha pili.
Chanzo kilipoulizwa kama mheshimiwa ana mpango wa kwenda kumripoti mtu huyo kwanye kitengo cha Makosa ya Mtandaoni (Cyber Criminal) kilisema:
"Kwa hilo mimi siwezi kujua. Mwenyewe anajua. Ila nimeyaongea yale ambayo nayajua tangu mwaka 2025 wakati wa Kura za Maoni ndiyo hiyo audio ilitengenezwa ili kumchafulia kwenye mchakato wa ubunge ndani ya chama."
KWA NINI SAUTI ITOLEWE SASA?
Chanzo kimeendelea kusema kuwa, sauti hiyo iliwahi kurushwa mara moja mwaka jana, kisha ikapotea. Kwa hiyo kurudiwa tena mwaka huu, mwezi Juni kunaashiria mkakati wa kumchafua mheshimiwa umerudi tena.
"Unajua siku za karibuni mheshimiwa Shabiby amekuwa akiwashukia mafisadi bungeni. Kwa hiyo inawezekana ni mpango mkakati wa kumtisha ili akae kimya au aache kuwaandama mafisadi na wala rushwa.
"Hakuna fisadi anafurahia 'spana' anazopiga mheshimiwa. Na kwa sababu adui yake anajulikana, ni rahisi sana kuungana na mafisadi kumkabili mheshimiwa ili tu wananchi wasema kumbe na yeye siyo msafi," kilimaliza
Chanzo.