ndugu "kijakazi", umenivunjia heshima sana. sina hakika una maana gani na neno "mbumbu" ila kama ni kwenda shule, mimi nafundisha chuo kikuu - computer science. kama bado nastahili kuitwa mbumbu leo, nachelea nitawaambukiza watoto wenu. kijakazi, naomba kazi ya kufagia nyumbani kwako.
Tatizo ni kuwa, simu ilikuwa inasema ni sikukuu ya "January 12" wakati pamoja na umbumbu wangu, nilikuwa na hakika ijumaa ilikuwa "June 6". Hii ikapelekea mimi kuwa na hakika kabisa kuwa hapo ubalozini kuna uzembe mkubwa unaendelea. na ndio sababu ya kutafuta namba zingine.
Sasa kama wewe unaona ni kwanini sikuamini kuwa ilikuwa sikukuu ya January 12, basi wewe una akili sana. wewe sio mbumbu.
ukiangalia huyu mgeni hapa "uniquetanganyik" (see post #17 in this thread) amenifahamisha June 7, ameandika
"Nadhani tatizo ni kuweka wrong date kwenye answering machine" nami nimemshukuru sana. mi nimefurahi kuwa hata mtanzania aliyeko huko (yaani uniquetanganyik) amekubali kuwa tatizo lilikuwepo.
na pamoja na kuniita mimi mbumbu, ila ujue through my post, JF imepata member mmoja aliyejiunga kujibu hoja yangu (hii post #17 ndo ilikuwa post ya kwanza ya uniquetanganyik). namkaribisha na namtakia kila la kheri alete hoja zenye msingi kama alivyojibu hoja yangu. kwani alielewa kuwa mi nahitaji kueleweshwa, na huu ni mwanzo mzuri.
niliwashauri wale jamaa watume maombi ya Denmark na naamini watafika hapa (ofcourse kuongeza hela kwenye mzunguuka wa shilingi yetu).
ujue ijapokuwa mimi ni umbumbu lakini, hata website yao haikusema kuwa ni siku kuu na wana simu kibao (ofcourse tunaendelea kuzi-audit hizi simu zote ili tuone za kweli ni zipi tufikishe taarifa kunakohusika). haya mambo ya ICT ndo professional yangu ya kimbumbu hivyo nitashauri kimbumbu mbumbumbu hivyo hivyo.
hii website yao wametumia Joomla! CMS kuijenga. lakini URLs zote sio Search Engine Optmised (SEO) URLs zina alama za sawa sawa
(mfano: http://www.tanemb.se//index.php?option=com_content&task=view&id=32&Itemid=58) wakati moja ya sifa yake kuu hii Joomla! CMS ni kuenable SEO. kwa ilivyojengwa kimbumbu webiste hii sasa hivi sio rahisi kuzi-google information zake.
huu ni umbumbumbu pia kwani kila mtengeneza website lazima ajue njia rahisi ya watu kujua kilichoko kwenye website yake ni kupitia googleling. hizi url watu huwa hawazikumbuki sana, au sio jamani au naendeleza umbumbu hapa?