Aibu, Ghana ilijenga Pokuase flyover kwa dola 94M wakati Tanzania imejenga daraja la Kijazi kwa dola 100M. Wote walitumia mikopo. Fananisha picha

Unakuta aliyeleta uzi hana ufahamu na maswala ya Uhandisi, Manunuzi na Uchumi kwa Ujumla.
Mkuu mimi ni mhandisi mwandamizi katika sekta mojawapo hapa nchini baada ya kutoka kwenye nchi moja iliyoendelea.
 
Kama limemaliza tatizo la folen bas wamefanikisha malengo, swala la pesa kupigwa hata ww ukipewa kandarasi ya kujenga hata nyumba huwez ukatumia pesa zote ulizoomba ktk bajeti.
 
Mkuu mimi ni mhandisi mwandamizi katika sekta mojawapo hapa nchini baada ya kutoka kwenye nchi moja iliyoendelea.
Mkuu basi kwa namna hiyo unatuangusha sana Wahandisi, Projects huwa zinavary kutokana na eneo n.k, upatikanaji wa materials, expertise, mambo ya Tendering n.k
 
Mkuu basi kwa namna hiyo unatuangusha sana Wahandisi, Projects huwa zinavary kutokana na eneo n.k, upatikanaji wa materials, expertise, mambo ya Tendering n.k
anatuangusha hakika,,
 
Mkuu basi kwa namna hiyo unatuangusha sana Wahandisi, Projects huwa zinavary kutokana na eneo n.k, upatikanaji wa materials, expertise, mambo ya Tendering n.k
Mkuu kwenye hili bandiko nimekuangusha vipi? Kwa kuangalia ni aibu kujenga daraja pale ubungo badala ya kujenga flyover.

Hapo ghana wamejenga kwa namna ambayo hakuna foleni hata kidogo. Kijazi pale bado kuna taa. Kijazi pale hakuna any special engineering design, ni straight construction.

Gharama sio issue sana kwasababu ya dynamics mbalimbali lakini kwa akili ya kawaida kabisa kuna namna hiyo project ilikuwa highly overpriced.
 
Achana na maswala ya kukariri me nachofahamu hizi ni nchi mbili tofauti inawezekana Ghana walitoa msamaha mkubwa wa kodi. Hata upatikanaji wa raw material hatuwezi fanana.

Nachojua Ubungo hakuna folleni tena. Hongera kwa wote waliofanikisha mradi huu mkubwa ulio tatua changamoto kubwa

Mungu awabariki
 
Zote zimejengwa kati ya 2017 na 2021.

Pale Kijazi hakuna any special engineering design, ni straight construction. Huwezi kufananisha na hiyo kazi nzuri waliyofanya ghana.
Kumbe wewe ni mtaalam wa haya mambo?
 
Kumbe wewe ni mtaalam wa haya mambo?
Ndio, ni mtaalamu na ndio maana naona kuna jambo halipo sawa. Bora hata fedha ingetumika nyingi zaidi lakini kazi iwe ya kuvutia.

Kulikuwa na sababu gani kujenga daraja na bado kuwa na mataa?
 
Alafu wakagawana hayo madaraja kwa kuyapa majina yao kama walivyogawana 10%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…