gbrother
JF-Expert Member
- Mar 22, 2011
- 408
- 51
Nimesikitishwa sana sana na uamuzi wa TFF jinsi mlivyofanya kwa hayati Sylvester Marsh, Hii ni aibu ya mwaka na kushindwa kusamini mchango wa wapigania soka katika nchi yetu.
Marsh alikuwa kocha msaidizi wa Timu ya Taifa kabda ya umauti kumkuta, ukiacha ilo alikuwa na mchango mkubwa sana katika kukuza soka la Tanzania na ndio maana kwa inavyosemekana TFF mlikuwa mnajiandaa kuingia nae mkataba awe kocha mkuu wa timu ya vijana, Ili linaonyesha ni jinsi gani mlivyokuwa mnakubali kazi yake, na ndio maana amkusita kumwomba aje awanoe vijana wadogo, maana huku ndio msingi wa maendeleo wa soka la vijana.
Cha ajabu mmeshindwa kuusafirisha mwili wake kwa kuangalia hadhi aliyonayo, mwanza pana umbali sana, lakini mmeona mwili wa jemedali wetu muusafirishe kwa eti wenyewe mnatupoza na kuita gari maalum, yaani ndege zote hizo zinazoenda mwanza kwa kukosa fadhila, na ubahili wa kibinafsi wa hela (maana najua kuna viongozi watasafiri tu ndege wakijidai wanawahi msiba) mnasema eti mmekosa ndege.
Hii ni dhambi, tena dhambi kubwa,
Hatukatai kwa usafirishaji wa maiti kwa basi kutoka dar kwenda mwanza, lakini kwa hadhi ya Marsh hakustahili mwili wake ukimbizwe kwa masaa yote hayo barabarani wakati usafiri wa anga upo, kuna Fastjet, Precision, na hata private jet ambazo kwa uwezo wenu mngeweza kupata,
Imeniuma sana na nitalia milele mpaka pale mtakapotubu kwa kosa hili.
Pumzika kwa amani kocha wangu kipenzi Sylvester Marsh