Aibu hii TFF hamuwezi kuikwepa

Aibu hii TFF hamuwezi kuikwepa

gbrother

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
408
Reaction score
51
Nimesikitishwa sana sana na uamuzi wa TFF jinsi mlivyofanya kwa hayati Sylvester Marsh, Hii ni aibu ya mwaka na kushindwa kusamini mchango wa wapigania soka katika nchi yetu.

Marsh alikuwa kocha msaidizi wa Timu ya Taifa kabda ya umauti kumkuta, ukiacha ilo alikuwa na mchango mkubwa sana katika kukuza soka la Tanzania na ndio maana kwa inavyosemekana TFF mlikuwa mnajiandaa kuingia nae mkataba awe kocha mkuu wa timu ya vijana, Ili linaonyesha ni jinsi gani mlivyokuwa mnakubali kazi yake, na ndio maana amkusita kumwomba aje awanoe vijana wadogo, maana huku ndio msingi wa maendeleo wa soka la vijana.

Cha ajabu mmeshindwa kuusafirisha mwili wake kwa kuangalia hadhi aliyonayo, mwanza pana umbali sana, lakini mmeona mwili wa jemedali wetu muusafirishe kwa eti wenyewe mnatupoza na kuita gari maalum, yaani ndege zote hizo zinazoenda mwanza kwa kukosa fadhila, na ubahili wa kibinafsi wa hela (maana najua kuna viongozi watasafiri tu ndege wakijidai wanawahi msiba) mnasema eti mmekosa ndege.

Hii ni dhambi, tena dhambi kubwa,

Hatukatai kwa usafirishaji wa maiti kwa basi kutoka dar kwenda mwanza, lakini kwa hadhi ya Marsh hakustahili mwili wake ukimbizwe kwa masaa yote hayo barabarani wakati usafiri wa anga upo, kuna Fastjet, Precision, na hata private jet ambazo kwa uwezo wenu mngeweza kupata,

Imeniuma sana na nitalia milele mpaka pale mtakapotubu kwa kosa hili.

Pumzika kwa amani kocha wangu kipenzi Sylvester Marsh
 
Mungu ni mwema, TFF mlitafakari hili kwa kina leo yeye kesho nyie.....malipo ni hapahapa Duniani
 
Wameshindwa hata kupitisha harambee watu tujitolee visenti vyetu??!!!
Ni roho mbaya na ubinfsi tu, na hii imeanzia wizara husika sio TFF tu.

Aibu sana na inakatisha tamaa kabisa. . . .
Mungu ailaze roho ya mwalimu kwa amani. . . .

Aamin
 
una roho mbaya sana wewe malinzi nilishangaa sana nilivyoona habari star tv..kwel kocha kama yule apigwe na upepo mpk mwanza? umenikera snna wewe
 
Miaka ya zamani watu walitembea kwa miguu tu, hakukuwa na baiskeli wala toroli na maisha yalienda, yakaja mabaiskeli na matoroli, magari na hizo ndege na merikebu, tusidharau gari kwa ujio wa ndege.

Heshima ya kuupeleka mwili wa kocha kwao mwanza kwa maziko ndio subject ya utu wetu, tumeubeba mwili kichwani all the way to mwanza, au tumeupakia kwenye mkokoteni ni ufahari wetu tu. Kumbukeni FAHARI NI MAMA WA UJINGA.

Tukutane mwanza tafadhali kwa maziko ya kocha, mtakaopanda ndege sawa, mtakaotembea kwa miguu sawa, mtakaokwea "mapipa ya tanga na sumbawanga" njooni tumzike kocha.
RIP COCHA
 
Jamani tusiwe wepesi wa kulaumu tu na kuanza kuwaombea mabaya wengine. Kikubwa ni mwili ufike Mwanza na upumzishwe kwa amani. Tunafundishwa kushukuru kwa kila kitu, ukipata kidogo unashukuru, ukipata kikubwa unashukuru zaidi.

Nenda kwa amani Sylivester Marsh, kutangulia kwako isiwe sababu ya malumbano.
 
Walau tff ningewaona wa maana iwapo wangesema ukweli wana kiasi fulani kisha wadau wengine kama azam (aliwahi kuwa kocha wao), wachezaji aliowahi kuwafundisha kwenye academy yake pamoja na timu za taifa, wizara ya michezo pamoja na wadau wengine wangeongeza pale tff walipoishia. Watz ni watu wenye moyo wa kuchangia mbona hiyo pesa ya kumsafirisha kwa ndege ingepatikana fasta. Inawezekana kabisa tff walikuwa hawana pesa ya kumsafirisha kwa wakati huo (japo sitaki kuamini hilo) kwani msiba wenye umetokea ghafla sana. Lakini hata kuratibu michango tff imeshindwa?
 
Nianze kwa kurudia kutoa pole kwa makocha,familia ndugu na jamaa wa marehemu Marsh.Mchango wa Marsh katika maendeleo ya mpira kuanzia akiwa mchezaji hadi kocha ni wa kuenzi daima.
TFF kwa kushirikiana na makocha tuliuchukua msiba huu ukawa wa kwetu.Zaidi sipendi kuyaongelea maisha binafsi ya marehwmu maana katika hali ya kawaida familia ya marehemu ndio ingetuongoza katika kutoa maamuzi muhimu kuhusu taratibu za msiba,usafirishaji wa mwili na maziko.Ilibidi tuchukue maamuzi ambayo kusema kweli kiutaratibu na kwa mila zetu za kiafrika hatukustahili kuyachukua.
Usafiri wa kupeleka mwili mikoani kwa Coaster ni wa kawaida kabisa hata kwa familia zenye uwezo.Mimi mwenyewe nimesafirisha marehemu wengi ndugu zangu kwenda Bukoba kwa Coaster,it is a normal practice.Kutoka Dar kupeleka maiti Moshi Iringa Songea Tanga Mwanza nk kwa Coaster ndio utaratibu wa kawaida kabisa.Uzuri wa Coaster ni kuwa ndugu jamaa na marafiki nao wanapanda gari hilo hilo na marehemu,wanamuimbia mapambio na kumuaga njia nzima.Ubaya ungekuwa kama TFF tunge abandon maiti Muhimbili.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF wamechangia msiba huu,makocha wamechangia msiba huu.TFF imewakilishwa mazikoni na mjumbe wa Kamati ya utendaji Lufano,Mkurugenzi Madadi na uongozi wa chama cha mpira Mkoa wa Mwanza.
Tumuache mwenzetu apumzike kwa amani,tusiingize siasa za mpira kwenye jambo zito kama hili.
RIP Marsh
 
asante sana mwenyekiti kwa kutupa maelezo haya juu hapo, lakini bado nashindwa kuyaafiki hayo usemayo hapo juu, maana kwenye habari ya star tv kuna kiongozi (kama sio wewe) alisema mlikosa ndege ya kusafirisha mwili, na ukiangalia kwenye post yangu hapo juu nimeliongelea ili, sasa hii dhamila ya kusema kwa coaster ilikuwa ktk mfumo huo usemao, bado nashindwa kupata nia ya dhati ya ukweli huo
 
Back
Top Bottom