Aibu: Kama data hizi za BOT ni za kweli basi Rais Magufuli na serikali yake hawana faida kwetu

Aibu: Kama data hizi za BOT ni za kweli basi Rais Magufuli na serikali yake hawana faida kwetu

Vumilieni ,siku mtashuhudia profesa mmoja akitumwa kuandika kitabu chenye hasi na chanya kiutendaji akikaribia kufa
 
Nilimsikia waziri anasema, hatuwezi kumpangia mkulima bei ya mazao kwani kahangaika mwenyewe kwenye kulima, kununua mbegu, mbolea, kupalilia, nk. na kwamba anayeona vyakula vimekuwa bei juu na yeye akalime, nikajiuliza hivi huyu ni waziri kweli. Hivi dakatari akiamua kufanya consultation fee kwa laki tano, injinia naye aseme nahitaji milioni 5 kuniona kisa alihangaika mwenyewe kwenda shule, kupiga umande, kuchapwa viboko, kubeba kuni, kulima shamba la shule, kusoma mavitabu makubwa hadi kukesha hiki kijiwe kitakalika kweli?
 
no vision no mission.

kiufupi ni hivyo tu.
 
"Nawashusha walioko juu nawaweka size ya kati,
Nawashusha waliko chini nafukia ardhini" By Lord Eyes
 
Ni hatari sana kuuingiza Ugali (mahindi) kwenye soko huria aisee ni hatari...ni hatari kubwa!!

Yaani ugali ndiyo kila kitu...
Ni balaa, nasema huyu bwana atameza matapishi yake, subirini
 
Kilo ya unga wa sembe umeshafika Tsh. 1600/=... Kwa Hali hiyo sitoshangaa ikifika Tsh 2000 mwezi ujao...

Yaleyale ya mtikisiko wa Bei ya sukari na korosho yanajirudia..
 
Kitu asichokijua ni kwamba mazao yote kwa sasa yako kwa wafanyabiashara. Anapotetea mazao yauzwe kiholela bei yoyote anawanufisha wafanyabiashara siyo hao wakulima wanyonge. Napendekeza bodi ya mazao ifutwe tu maana haina kazi ya kufanya tena maana wafanyabiashara watajipangia bei za mazao wanavyotaka, hii ndo Tanzania
 
hii awamu ya tano kwa nini haipendi hata kujza ghala la taifa wao kwetu kumpiga kikwete vijembe na kujifanya wamefanya maajabu kumbe ni in a negative way.angalia akiba ilivyoporomoka TOKA TANI 452,000 MWEZI MARCH 2015 HADI 78,000 MARCH 2019,KWA NINI HANUNUNI VYAKULA NA KUJAZA MAGHALA,WANA PLAN GANI HAWA WATU?😡😕🙁
NFRA ilikuwa Ni price stabilizer, Bei ya nafaka ikishuka Sana wananunua mazao nakuyahifadhi, yakipanda Bei sana wanayauza kwa Bei nafuu, Sasa hii ya kukausha kihenge ndio kwanza naona
 
Hizo data zimepikwa na maadui wa taifa letu
Ingia website ya BOT ujionee, unafikiri jiwe ni mjinga alivyosalimu amri na kusema wakulima wajipangie bei?
kujipangia bei unafikiri itapanda ama itashuka? nani mwenye nguvu ya mazungumzo wakati wa kununua?

huu ujinga wenu ndio mnaoutumia kumpa phd ya "kuua viwanda" hapa Tanzania.

Wanunuzi ni wachache sana, yupo

1. Mo dewji.

2. Bhakhresa.

3. Pembe.

4. Abdul khadir.

Hao wanafahamiana, wanapanga bei ya kununulia, hamtaki kaleni hayo mahindi mpate afya!
 
Kuna hii taarifa
IMG_20191121_060059.jpeg
 
Mtoa mada vyovyote vile ilivyo lakini nchi inasonga tu. JPM na serikali yake wanajitahidi kufanya yale wanayoweza tena ndani ya muda mfupi tu. Yapo yanayoyumba lakini mazuri ya kutosha tu yapo mengi sana.

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom