Mi nimewahi kupeleka CV mahali, huyo Boss kaniambia sawa tutakupigia. Sijavaa kimtego wala nini, wala sina kitu cha kumshtua mtu kivilee mi wakawaida kabisaaa!!!
Ilikuwa siku ya Alhamisi, jumamosi yake asubuhi akanipigia akaniambia mm ni yule Boss wa sehemu fulani, hebu tukutane Rose garden kuna jamaa watakuwa pale saa kumi tuongee ongee kuhusu ile CV yako. Nikasikia moyo unanienda mbio, nikafikiria CV Rose garden kweli? Basi nikajilazimisha tu nikaenda nimevaa kama natoka kanisani yani. Kufika nikamkuta kakaa peke yake ananisubiri.
Akaanza kazi utapata usiwe na wasiwasi kabisa, mabinti mnao onekana waaminifu kama ninyi hamwezi kukosa kazi kabisa. Hapo macho yote yananikodolea kama nini, mara kaanza ngonjera zake ooh mi nilikupenda sana binti una adabu khe.........kilichoniokoa hapo nilimwandikia ndugu yangu mmoja msg kaja kunifata nikamkimbia kwa kumwambia tunaenda kwenye msiba. Nikajuta kudiscus CV baaaaa........dah mpaka leo hajawahi niitia hiyo kazi.....sijui alichoma moto nakala zangu.....