Aibu kuu kwa nchi yangu Tanzania huko Saudi Arabia: Bondia apigwa kipigo cha mbwa koko

Aibu kuu kwa nchi yangu Tanzania huko Saudi Arabia: Bondia apigwa kipigo cha mbwa koko

Na hii ndiyo watanzania wajue Hassan Mwakinyo kuweza kuhimili raundi kumi na kuibuka mshindi siyo swala jepesi, tusipende kubeza jitihada za watanzania wenzetu!
Haina uhusiano mkuu. Hawa mabondia sio fani yao, Mwakinyo kama ajifue zaidi. Mjue kuwa kutiliwa shaka ni faida kwa Mwakinyo kuliko kulewa sifa. Joshua pia alikuwa hivyo pambano la kwanza dhidi ya Ruiz ndipo akapigwa. Kifupi Mwakinyo awe tayari kukubali challenge na kujifunza kujibu kwa vitendo.

Kuhimili kweli alihimili lakini matokeo ndio yanayotiliwa shaka
 
Bondia wa Tanzania aitwa Seleman Said, amepewa kipigo cha paka mwizi raundi ya kwanza kwa knock out kutoka kwa bondia wa Marekani.

Shindalo ili ni shindano la utangulizi kabla la shindano kati ya la Joshua na Ruiz ambalo linafanyika leo hii. Bondia wa Tanzania alipigwa ngumi nzito ambayo ilimfanya apoteze fahamu na kuletewa mitungi ya hewa ya oxygen.

Baada ya kupata nguvu na kusimama refa aliamua kumaliza mchezo huo na kumpa ushindi bondia kutoka marekani. Mchezo unaofatia ni wa Joshua na Ruiz. Pia katika mshindano haya ya leo kuna bondia wa Tanzania mwingine kwa jina anaitwa Mohamed Swedi nae alipigwa kwa knock out bila msaada wa refa tungesikia mengine.
Bondia wa Tanzania alipigwa ngumi nzito ambayo ilimfanya apoteze fahamu na kuletewa mitungi ya hewa ya oxygen. [emoji23][emoji23]
 
Mbona Anthony Joshua alipigwa na jamaa lenye kitambi, tumbo kubwa huku yeye akiwa na six pack yake, mrefu, mwili umegawanyika. Alitudhalilisha sana watu warefu. Leo naona wameamua kumzawadia ushindi.

Huyo mtanzania nasikia kapigwa ngumi moja ametapika dagaa ulingoni. Tumpe pole. Atakua anatokea pwani.
Kama alitapika dagaa basi atakuwa wa kanda ya ziwa... Maana kama angekuwa muha basi asinge kubali kirahisi...
 
Ubaya wa kichwa huwa hakina mazoezi kwa waliowahi ona mapambano ya Mike Iron Tyson na mabondia kama, Clifford Etienne,Bruce Seldom na wengine wengi, hawastajabu sana bondia yoyote kuchapwa mapema
 
Wapambe wa kusifia kila zuri hutajwa likifuatiwa na 'serikali ya tano chini ya mh..' , mbona sijaona hili liitwalo la aibu likihusiswa nao? Au ni wapinzani wamehusika?
 
Mambo mengne kwa watu wengine unakubali tuu point za mezanii. Mimi ukinipapasa tu nikasikia upepo namkimbilia refa atangaze ushindi.
Ya nn kufaaa?

Umenikumbusha kale ka clip ka Charlie Chaplin ka ulingoni.

Hahaaa nachekaga sanaaaa, ngumi moja tu wenge nusu saa.
[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Back
Top Bottom