Aibu kuu: Uongozi wa Hersi/Arafat ni lainilaini sana, mnakosea

Aibu kuu: Uongozi wa Hersi/Arafat ni lainilaini sana, mnakosea

njaakalihatari

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2019
Posts
4,081
Reaction score
8,671
Hii siyo yanga ninayoijua, kuwa upande wa mwenye mapesa siyo kigezo cha kuweza uongozi, yanga ni ngangari tangu enzi hizo siyo watu wa mchezomchezo muulize Iman madega na wenzake waliowahi kuvamiwa nyumbani kwao, watu shakula bakora sanaa pale jangwani

Sasa jana afisa mkubwa wa klabu aliyewaletea ubingwa baada ya miaka 4 anafungiwa kiuonevu kabisa nyie mnatoa statement ya kiutopolo iliyolegea kama mlenda?

*Morale ya wanayanga nchini kote ipo juu kupigania haki ya mwenzao kindakindaki anayeipenda yanga toka moyoni yaani Hajj manara

*Wachezaji na benchi la ufundi wako tayari kupigania haki hiyo,mbona mwakalebela aliwahi kufikiria kuihamishia team zanzibar nyie mnashindwa nini?

CHA KUFANYA SASA
* Simamisheni shughuli zote za club, kuanzia kesho wachezaji na benchi la ufundi waende pale karume na mabango kushinikiza msemaji bora kabisa aliyesababisha ligi ya bongo kuingiza teams 4 afrika aachiliwe huru

* Kuwe na maaandamano non stop ya mashabiki wa yanga kufunga mitaa ya msimbazi,kariakoo hadi karume hakuna shughuli ya kiuchumi kufanyika hadi mwanayanga kindakindaki manara aachiwe

* Anzeni plans za kuhamia ligi ya zanzibar

Halafu Arafat umekuwaje kumbuka ulikuwaga mtu wa misimamo sana kama ulivyosikitika soka la bongo kumkumbatia chizi morrison mbona kimya tena?

arafat hajj.jpg
 
Mkifanya undava kuingiza mambo ya siasa kwenye issue za wazi za kimichezo mtafungiwa kama Kenya na Zimbabwe.
 
Hii siyo yanga ninayoijua, kuwa upande wa mwenye mapesa siyo kigezo cha kuweza uongozi, yanga ni ngangari tangu enzi hizo siyo watu wa mchezomchezo muulize Iman madega na wenzake waliowahi ...
Naunga mkono hoja haiwezikani Haji Manara ambaye hata damu yake ni kijani na njano anaonewa kiasi hiki halafu hakuna tamko la kuisimamisha nchi? Siyo Yanga ninayoijua mimi. Yanga iliyoweka kambi nyumbani kwa mwenyeki Lloyd Nchunga hadi akabwaga manyanga
 
Naunga mkono hoja haiwezikani Haji Manara ambaye hata damu yake ni kijani na njano anaonewa kiasi hiki halafu hakuna tamko la kuisimamisha nchi? Siyo Yanga ninayoijua mimi. Yanga iliyoweka kambi nyumbani kwa mwenyeki Lloyd Nchunga hadi akabwaga manyanga
inasikitisha sana kwanza wasimamishe shughuli zote ikibidi wajitoe michezo ya CAF ili karia ajue wako serious. Manara kafungiwa akiwa anaipambania team yake anayoipenda tangu utotoni lazima wana yanga wampiganie
 
Walete ndonga zao tufungie team nzima...na bdo tupo kweny mchakato kuna makanjanja yanayojiita wachambuzi wa mpira....soon wataitwa kweny kamati ya maadili
 
Back
Top Bottom