Aibu Kwa waangalizi Senetor John Kerry, Rais Thabo Mbeki na Rais John Mahama

Aibu Kwa waangalizi Senetor John Kerry, Rais Thabo Mbeki na Rais John Mahama

Uchakachuaji haukuwa kwenye vituo vy Kupigia kura(ambako ndio prime target ya observers)..uchakachuaji ulitokea kwenye kujumlisha kura tena electronically...ambapo observers hawakuwa na access napo.
Zoezi la upigaji kura lilikuwa fair kabisa..na observers walichoripoti kilikuwa sahihi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mtazamo wangu uchaguzi kwa kiasi kikubwa ulikuwa huru na wa haki. Kasoro ndogo zilizojitokeza hazikuwa na uzito wa kupotosha maamuzi ya wakenya kwa ujumla wao.
Kama unachunguza siasa za Kenya opinion polls nyingi za nyuma zilionyesha Uhuru akiongoza kwa asilimia zile zile 51-54%. Sababu kubwa ni siasa za ukabila Kenya , na matokeo yalitabirika.
Tatizo lingine ni kwamba hata mahakama nayo ina dalili za ukabila au kushindwa kusimamia haki. Kama alivyosema Prof Lumumba, NASA hawakuwa na ushaidi wa zaidi ya shutuma katika Kesi yao. Tusubiri written judgement ili tuone kwa mapana.
Bado sielewi kwa nini shutuma ziwe kwenye transmission ya forms za matokeo, wakati NASA walishiriki kukagua form originals. Na hizo forms chache ambazo wao wanadai zilikuwa hazina sahihi za returning officers zilionyesha Odinga akiongoza, hivyo haziwezi kuwa za kufoji.
Raila anatumia njia ya "vuruga penye uhalali wa kushindwa ili nitafute upenyo wa kushinda kwa nguvu". Alifanya kuikataa tume iliyopita bila sababu zozote za msingi. Akaanzisha vurugu hadi tume ikavunjwa. Kwenye kampeni akasema nikishinda nitakubali matokeo nikishindwa sitakubali. Baada ya tume kutangaza matokea akadai ameibiwa kwenye transmission, tume kwa busara ikakubali kura zihesabiwe kwenye forms originals, nako akashindwa.
Kwanza akasema sitaenda mahakamani sababu alijua hawezi shinda kesi, baadaye akajaribu kulazimisha na kwa mshangao wa watu makini ameshinda.
Kitakachotokea, atalazimisha kuundwa kwa tume nyingine na atajitahidi ili awe na watu wake na nabashiri atacheza faulo na akishindwa ni vurugu Kama kawaida yake.
 
Back
Top Bottom