Aibu Old Trafford, Bournemouth yaipiga Man. United 3-0

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Uwanja wa Old Trafford umekuwa mchungu kwa wenyeji Manchester United baada ya kukubali kichapo cha magoli 3-0 kutoka kwa Bournemouth katika Premier League.

Kipigo hicho ambacho ni cha 7 katika mechi 16 za United katika EPL 2023/2, kimekuja siku moja tangu Kocha Erik Ten Hag na Harry Maguire wa United wapate tuzo ya Kocha Bora na Mchezaji Bora wa Mwezi.

Aidha, nahodha wa Man United, Bruno Fernandes amepewa kati ya njano katika mchezo huo, hivyo ataikosa mechi inayofuata dhidi ya Liverpool.
 
Huyu fala Man U kesho kutwa aende akamalizane na Bayern haraka haraka atimkie zake europa huko maana huku uefa ni kichefu chefu tu.
 
Ifike hatua itoshe kusema Manchester United imekuwa ni mahali au kundi la watu /uongozi usiojua ni kina nani wanafurahi au kuhuzunika kwa matokeo ya namna yoyote aidha ushindi ,sarw au Kushindwa .Navumilia lakini inauma sana .
 
ama aibu ya mwaka
 
man utd anaweza kula mkono kwa yanga
 
Huyu mtoa mada itakuwa mgeni na man u, yaani man u kupigwa inakua aibu, sasa hizo aibu si kila siku
Eti anashangaa man united kufungwa πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…