LGE2024 AIBU: Tanzania bado watu Wanajisaidia Vichakani. Uchaguzi wa 2024 uwe Mkombozi ili kulinda Mazingira

LGE2024 AIBU: Tanzania bado watu Wanajisaidia Vichakani. Uchaguzi wa 2024 uwe Mkombozi ili kulinda Mazingira

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam Wakuu,

Ni aibu kubwa baada ya miaka 60 ya uhuru kuona Watanzania bado Wanajisaidia Vichakani.

Hii inatokana na kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa Wasiowajibika.

Uchaguzi wa 2024 uwe Mkombozi ili kulinda Mazingira kwa kuhakikisha tunachagua Viongozi wanaojielewa bila kujali wanatoka chama gani.

Pia soma: DOKEZO - Serikali inasema Kipindupindu Simiyu ni ukosefu wa Vyoo lakini kuna sababu kubwa nyuma ya pazia

Kwa Mjibu wa Serikali ya Tanzania, asilimia 13.4 ya Wakazi wa vijijini hawana vyoo kabisa. Tafsiri yake ni kwamba watu hawa ndiyo wanaojisaidia ovyo (Open defecation) vichakani na maeneo mengine ambayo sio rasmi.

Hali hii inachangia kuwepo kwa magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu. Ambacho kinaua.
Kipindi cha Januari hadi Oktoba 2023 jumla ya watu 749 waliougua kipindupindu 16 kupoteza Maisha.

Watu wanapoteza maisha kwa Uzembe wa mtu mmoja ambaye kapiga kura kwa kupewa Rushwa nk.

Ni wajibu wetu sasa tuchague Viongozi ambao watasimamia kikamilifu swala la Mazingira ikiwemo Ujenzi wa vyoo.

Pia soma:
 
Back
Top Bottom