Aibu: Yanga inabebwa Taifa

Mpira wa bongo wote tu ni bado sana.
 
Nenda Kalimie meno....Yanga ni Umoja wa Mataifa.....Thanks 4 EU...nyinyi si Sembe Kantri....
 
Uli
Tukuelewe kwanza kabla ya kuanza mjadala. Uliowapinga kuwa wanashangaa timu mbovu kuongoza Ligi ulipinga kipi? Ulipinga mshangao wao, au ulipinga kwamba Yanga si timu mbovu, au ulipinga kwamba Yanga haiongozi Ligi? Na je, mechi moja uliyoiona wewe na ukajiridhisha kwamba Yanga imebebwa na refa inatosha kukufanya ubadili msimamo wako, na ni sahihi sawa na kusema Simba kufungwa mechi moja na mbao ni timu mbovu?
Neno la kuambiwa ongeza na lako. Je, umeongeza lako ukaridhika kwamba Yanga ina kila sababu ya kubebwa licha ya kuwa haina hela, haina majina matukufu kwenye usajili wake, Malinzi aliyekuwa anaibeba na wenzake wako ndani, haichezi soka la kuvutia, viongozi wakuu wa TFF ni wadau wa Simba, yenyewe imekuwa ikilumbana na TFF tangu upangaji ratiba hadi uchaguzi wao? Na kama umeridhika kwamba kweli inabebwa licha ya hali hiyo, umeridhika kwamba mdomo wa Akilimali una sauti kuliko fedha ya Mo, kwamba si Malinzi na wenzake tu walio tayari kuibeba Yanga, kwamba hata wadau wa Simba ndani ya TFF ni vibaraka wa Yanga, na kwamba mvutano wa TFF na Yanga ni kiinimacho tu dhidi ya Simba? Na kama umeridhika hivyo, ndiyo unakubali kwamba Simba si chochote mbele ya Yanga, hata kwa mazingira gani?
 
Uandishi wako mbovu mtani chura.
 
Mechi ya Simba vs JKT Tanzania Erasto Nyoni Aliushika mpira mara mbili tofauti ndani ya 18 lakini refarii alitafsiri tofauti na simba walitoka na point 3 hakuna aliye lalamika kwakua ni sehemu ya mpira. Yanga leo wamepambana na walistahili ushindi.JKT waliamua wawe wanajingusha na wamepata matokeo rafiki.
 
Nkana huyoooo .....
 
Ulikuwepo uwanjani?

Kichaa gani wa kuibeba Yanga yenye "njaa"
Marefa pamoja na maagizo ya kuhakikisha Yanga inafungwa, lakini inapeta kwa juhudi na mpira wake.
Wakati qa Malinzi eti Yanga ilikuwa inabebwa. Wakati huu top brass ya TFF ni Simba. Bado Yanga inabebwa?
Mechi inapangwa saa moja. Ghafla inaridishwa saa kumi na wachezaji waupiga mwingi bila kula. Bado Yanga inabebwa.
Leo ratiba ya awali ilikuwa saa kumi. Ikaja saa moja, baadaye saa kumi na moja na hatimaye ikarudi saa kumi. Bado Yanga inabebwa.
Mambo mengine yataka moyo kuyaamini.
 
Naww subilia utabebwa
 
Agiza kande ule.
 
Ruvu shooting wamenyimwa penati 2 za wazi kabisa. Sijui refa alikuwa wapi. Hii ndio yanga mkuu, wanaaiita timu ya serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…