Aibuuu Emmanuel Mbasha amtongoza Carry aambulia cha mbavu

Aibuuu Emmanuel Mbasha amtongoza Carry aambulia cha mbavu

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Aliyekuwa mume wa Flora Mbasha aambulia aibu ya mwaka baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kupata penzi la DJ Carry au Carrymastori kama anavyojulikana na wengi .

Carry ametishia kuanika chats zao zote ambazo Emma alikuwa anamtumia Carry kulilia penzi la Carry licha ya mara kadhaa Carry kumkataa lakini jamaa amekuwa king'ang'anizi mpaka kero.

Hii ni aibu kwa kweli ,yani jitu zima badala ya kuhangaika na watu wa rika lake anahangaika na vitoto mpaka anaonekana kituko .

IMG_20190416_145131_549.jpeg
IMG_20190416_154714_475.jpeg


*************************************************"********* MANENO YA MBASHA
Kwa yanayoendelea sitaki kumlaumu sana @carrymastorr ila naweza kusema ni moja ya athari za ukuaji wa teknolojia haswa katika upande wa mitandao ya kijamii. Ni mitandao pekee ndiyo inaweza kukutanisha hadi na watoto wa mitaani wasiojua raha wala thamani ya mzazi, ila nje ya mtandao ni ngumu sana kukutana na watu kama carry.

Maana nje ya mtandao ndiyo kuna maisha halisi. Ndugu zangu siyo kuwa nadharau watoto wa mtaani hapana ila najaribu kuweka mambo sawa. Just imagine, ati mwanaume kama mimi ninayepewa heshima hadi na waheshimiwa, leo hii nitongoze mtu anaejulikana kama mbeya wa insta?! Hivi nitakuwa nimerogwa, au nimetupiwa jini?! Si hata waheshimiwa watanishangaa kwa jinsi nilivyopotea.

THE FACT IS.. Carry anahitaji kuongeza followers ili aweze kupata matangazo kwenye page yake na ndiyo maana katika post zake huwa anajaribu kuwa attack watu wenye majina makubwa pamoja na ushawishi kwenye jamii. Hii inaweza kuwa mbinu nzuri kwake ki biashara ila ni vyema akapata elimu kidogo ili awe na mipaka haswa katika mambo ya familia za watu.

Maana leo kaniganda mimi week yote, mara amsakame zariitheboss yote hii ni kukimbizana na ndoto yake ya kuingiza shilingi milioni tano kwa mwezi, jambo ambalo akifanikiwa kwake itakuwa ni hatua kubwa sana ki maisha maana hapo alipo hata milioni moja hajui inafananaje, na ndiyo maana anakuwa na afya mgogoro kama mtu anaeishi na nanihii mwilini.

Ujumbe wangu mzuri kwako carry, jitengenezee platform yenye kukuzalia matunda na sio kujitengenezea maadui wasiokuwa na sababu. Kama humjui baba yako au labda baba yako hakuweza kukutoa out za kibabe kama hizi ninazompigisha mtoto wangu ni vyema ukaomba msaada wasamalia wema wenye moyo wa kukutoa out. Ila hii ya kuumizwa na maisha mazuri ya watu wengine hili ni daraja la kwanza linalokupelekea kuwa mchawi kamili. Bora uokoke ili unenepe na roho mbaya ikutoke na unikome kabisa Carrymastory

Mwone Hata afya hakana sikapendi hivi kanagodoro kweli haka mana kamezidi,ngoja nikachane kilokole "Neno la Bwana kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.(Zaburi 110:1)

Maisha bila adui hayawezi kuwa maisha na raha ya mafanikio ni maadui waliokuzunguka. Hakuna binadamu ambaye hana adui, maana kila adui anaashilia uwepo wa Mungu katika maisha yako. Na endapo ukijipata hauna adui hii inaweza kuwa ishara tosha kuwa hauna Mungu. Maana dalili kubwa inayotambulisha mtu kuwa Mungu yuko upande wake ni kiwango cha maadui wanaoibuka na kukuchukia bila sababu.

Ndugu za Yusufu waligeuka na kuwa maadui zake baada ya kuwasimulia ndoto ambayo Mungu ameiweka ndani yake, hakuna alichowadhurumu wala kuwaibia bali future aliyokuwa nayo ndiyo ilisababisha achukiwe na kuingizwa kwenye matatizo, ambayo kwake yalikuwa ni mlango wa kumfikisha katika ndoto zake.Maadui wapo na hatupaswi kuwaogopa bali tunapaswa kumuomba Mungu atupe hekima ya kukabiliana nao. Ukisoma biblia kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi ufunuo utakuta sehemu kubwa tumefundishwa mbinu ya kuwashinda maadui zetu katika njia ambayo Mungu ameiridhia. Katika andiko nililolinukuu hapo juu ulikuwa ni unabii ambao Daudi aliutoa juu ya Yesu, miaka mingi kabla ya Yesu kuzaliwa.

Unaweza kuona maadui zake wanatabiriwa kuwapo hata kabla ya mimba yake kutungwa. Upendo tunaofundishwa katika maandiko ni moja ya mbinu ya kuwadhibiti Maadui kama carrymastory ili chuki zao zisije kukuharibu na kukukwamisha. Wanapokuchukia na kukupinga lengo lao ni kukutoa kwenye mstari, lakini unachopaswa kufanya ni kutojali zile chuki na kuendelea kupigania ndoto zako huku ukiamini kuwa Mungu atakufanikisha mbele ya macho yao. Na hivyo ndiyo kuketi mkono wa kuume wa Mungu,sasamimi kuwa karibu na Mwanangu wewe kinakuwasha kipi?? Carrymastory
 
[emoji16][emoji16]nilona jamaa mmoja amecoment hivi

"ila carry una kasura flani sio kabaya ila kachachuu"

[emoji23][emoji23][emoji23]wabongo bana.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ujinga tu, anatafuta kiki kwa lazima, kwani ajabu gani akitongozwa??Basi atakuwa anamzimikia jamaa kishikaj halafu nahisi jamaa alivyoona anazungushwa akaamua mtema, kanaumia roho sura yenyewe kama ya baba
 
Kama kamkatalia jamaa haina haja ya kumtangaza akaushe tu.
 
Back
Top Bottom