GE2025 Aida Kenani aaga wapiga kura Nkasi Kaskazini akisema, "sitasaliti mapambano"

GE2025 Aida Kenani aaga wapiga kura Nkasi Kaskazini akisema, "sitasaliti mapambano"

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Lissu kawaingiza chaka wenzake kususia uchaguzi. Huu ni uamuzi wa kipumbavu zaidi kuwahi kufanywa na chama cha siasa.
Hata wakishiriki na kuchaguliwa hawatatangazwa. Bora walivyo susia.
 
Aliyekuwa Mbunge pekee wa Chadema kutoka Nkasi Kaskazini, Aida Kenani amewaaga wapiga kura wake akisema kama atagombea hakuna wa kumshinda. Hata hivyo, amesema hawezi kusaliti mapambano.
Chadema imeweka msimamo wa kuzuia uchaguzi hadi mabadiliko yatakapopatikana, maarufu "No Reforms No Election."

Nimempenda Bure
 
Nakumbuka mara baada ya kutangazwq kuwa ameshinda alituambia kuwa hawezi kukiuka maagizo ya viongozi wake ambao walisema hamna kuingia Bungeni. Kilichofuata ni anakula kiapo cha ubunge! Alipoulizwa kulikoni, alisema hawezi kuwaangusha wapiga kura wake waliomtakq akawawakilishe. Kwa muda mrefu chama chake kilimtenga kwa sababu hiyo. Ila amekipigania sana chama chake. Anastahili kushukuriwa kwa hilo.

Amandla...
Uko sahihi, hata hivyo alipigana ndani ya bunge kibogoyo. Yaani ni bunge tulilolipuuza.
 
Back
Top Bottom