Mtaani pagumu jamani, muacheni mama akapige pesa za bwelele bungeni.
Wengi wenu humu hamjui mshahara wa mbunge ni million 14 kwa mwezi nje ya posho za kusinzia kwenye kiti, mkopo wa shangingi na pesa ya mafuta kila mwezi.
Dr Slaa alipoteuliwa kugombea Urais na Chadema alijuwa wazi hawezi kutangazwa mshindi, hivyo aliwapa Chadema condition kwamba analiachia jimbo la karatu lakini adiposhinda awe analipwa mshahara wa kibunge kwenye nafasi yake ya ukatibu mkuu.
Je Chadema kama chama kimempa offer gani huyu mama asamehe ubunge ili aunge mkono msimamo wa chama?
Na mkae mkijuwa huyu mama anajuwa vyema maslahi ya mbunge hass wa jimbo kwa sababu bunge lililopita alikuwa mbunge wa viti maalum.
Tuache mihemko turudi kwenye reality, January si mbali watoto wanataka school fees, acheni jamani, humu hakuna wa kuisamehe millioni 14 kwa mwezi mara miaka mitano plus mafao ya mwisho wa ubunge.
Acheni utani.