Uchaguzi 2020 Aida Khenani (CHADEMA): Siwezi kuwasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini, mimi ni mbunge halali, ninasubiri kuapishwa tu

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Chama kiliniamini kikarudisha mamlaka kwa wananchi na wananchi wamenipa mamlaka. Kama niliapa Chadema siwezi isaliti hali kadhalika siwezi wasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini.

Naomba nitoe msimamo wangu, mimi Aida nimechaguliwa kwa mujibu wa sheria na ni mbunge halali wa Nkasi Kaskazini, ninasubiri kuapishwa na hakuna jambo jingine, sina mabadiliko mengine.

Pia soma> Aida Khenan: Demokrasia ni muhimu kuliko ushindi wangu. Nipo tayari kuungana na wenzangu kwa maamuzi yoyote


Your browser is not able to display this video.
 
Hakika...

Demokrasia ni kuvumiliana...

Bunge lililopita,Spika mh.Ndugai alifafanua vyema yaliyowahusu wabunge waliofukuzwa na vyama vyao....tutaendelea kuona Spika akichukua hatua zilezile iwapo kutatokea KUFUKUZANA VYAMANI..

Kila la heri dada Aida Khenan,japo sijafurahishwa na kumshinda Mzee sahibu yangu mh.Ally Kessi,kwani tulikuwa na jambo letu Mimi na yeye kumlazimisha mh.Mwenyekiti wetu...yaani ATAKE ASITAKE....

All and all ninaheshimu AGREE TO DISAGREE na pia ninaheshimu demokrasia.

Best wishes,aamen
 
Hongera Kamanda wakuache, mbona kina Mbowe walikuwa wanakula hela za ubunge na wewe nenda ukapige hela, maana ukisusa hamna utakachokipata na huko 2025 kuna uwezekano kusiwe na hata siti moja ya wapinzani
 
Kama uchaguzi hautarudiwa sioni mantiki ya yeye kukubali wazo la kukataa ubunge, kawakilishe wananchi wako...huku tukiipambania demokrasia...ana familia na maisha ya kuishi licha ya gharama alizotumia
 
kama uchaguzi hautarudiwa sioni mantiki ya yeye kukubali wazo la kukataa ubunge, kawakilishe wananchi wako...huku tukiipambania demokrasia...ana familia na maisha ya kuishi licha ya gharama alizotumia
Uwakilishi bubu una faida gani? Atasikilizwa na nani bungeni akiwa peke yake? Hatakuwa na uwezo wa kupinga lolote lile liletwalo bungeni, sioni faida yeyote ile zaidi ya mafao tu!
 
..huyu dada aende bungeni.

..yeye na wananchi waliomchagua wameutolea jasho ushindi huo.

..kushiriki kwake bungeni hakuondoi ukweli kuhusu dhuluma kubwa iliyotokea ktk uchaguzi mkuu.
Huu ndo ukweli, namjua AIDA na nimekuwepo Namanyere tangu siku ya upigaji kura hadi kutangazwa matokeo, ilikuwa mbinde kweli kweli. Dada kapambana na majizi kwa nguvu hadi kunyang'anyana fomu za matokeo na Msimamizi wa kata ambazo baadaye zilijulikana ni feki. Mabomu ya mshindo zaidi ya 30 yamepigwa eneo la Halmashauri ya Nkasi kufukuza Wafuasi wake lakini walinawa maji na kujifunika vitambaa puani mapambano yakaendelea.

Mkuu wa Wilaya Said Mtanda na Mgombea wa chama chake walipita alfajiri tarehe 29/10 wakitangaza ushindi feki wa Ally Keissy, hali iliyowaamsha wananchi waliokuwa wanajua mshindi ni nani kuingia barabarani hadi Halmashauri kudai Mshindi halali atangazwe. Viongozi wa CHADEMA wanatakiwa kitumia busara kwa wale walioshinda, siyo kwamba wamepewa bure, wamepambana. Mbali ya kuwepo wizi lakini CHADEMA wamepata Madiwani 4 kati ya kata 17 baada ya mapambano makali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…