Aidha mbaki mnachambua Mchele au mkae kimya

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Tukisema Hakuna mnachojua muwe mnakubali. Tukisema mnaojiita Wachambuzi wa soka Tanzania ni washangiliaji kama alivyo Abdalla Saliboko wa Tandale na Oscar Maganga wa Sangamwalugesha muwe mnakaa kimya maana media zinazowalipa zinapoteza hela bure kulipa Wachambuzi Wenye hadhi Sawa na shabiki wa kawaida kiuchambuzi.

Ni zaidi ya SAA 12 tangu ligi Kuu ya NBC itamatike na kuzua utata wa Nani Mfungaji kiongozi Kati Said Ntibanzokiza na Fiston Mayele baada ya wote Jana kufikisha goli 17. Lakini Hakuna hata mchwambuzi mmoja aliyekuja na jibu sahihi kanuni zinasenaje? Wengine wanadiriki kusema sasa Kamati ya tuzo inakwenda kukaa ili itunge kanuni na kuja na jibu la Nani anastahili.

Hii itakuwa ni miongoni mwa maajabu ya soka. Kwamba Jambo litokee, ndo wanasheria wakae kutunga sheria/kanuni inayotoa majibu ya suala linalobishaniwa? Kama kweli ni wachambuzi tuonyesheni kanuni zilizopo zinasema nini?

Na kama hazisemi chochote kazi yenu katika kipengele cha kukosoa mliamwachia Nani? Basi njooni huku upande wa mashabiki tukae tusubiri wapishi wa sheria wakae watupatie msosi uliochemshwa Kwa dharura tubaki tunaharisha Kwa zamu.


 
Nimependa Sana KANUNI za Fifa za kombe la Dunia.

Endapo wachezaji watalingana kwa MAGOLi
Maamuzi YAFUATAYO yatafanyika.

1.
2.
3.
 
Ndio kwanza tff wametoa nafasi kwa wadau wa michezo wakiwemo hao wachambuzi kutoa maoni kuhusu kanuni. Kuwa na subira
Wacha-mbuzi hawahawa wasiojielewa watasaidia nini? Kwa hiyo TFF yenyewe haijui kanuni zake mpaka iwahusishe hawa Mbumbumbu?
 
Nimependa Sana KANUNI za Fifa za kombe la Dunia.

Endapo wachezaji watalingana kwa MAGOLi
Maamuzi YAFUATAYO yatafanyika.

1.
2.
3.
Kanuni za TFF za msimu uliopita zilikuwa zinakinzana na kanuni za Fifa ndio maana zikaondolewa msimu huu.

Kanuni za Fifa - Wafungaji wakilingana idadi ya magoli;
1. Mshindi ataangaliwa mwenye idadi kubwa ya assist
2. Wakilingana Assist, Ataangaliwa yule aliecheza michezo michache.
3. Wakilingana idadi ya michezo, wataangalia muda waliocheza (Amecheza dakika ngapi?)
 
Mimi katika hili nawaza natofauti, I think TFF mpaka sasa inajua ni kanuni ipi itatumika kuamua hili ila wameamua kutolisema mapema kwa malengo makuu mawili.

1) Lipate artime kubwa ili jambo lingine lilokua na airtime likae kando

2) Siku ya kutoa tuzo Wananchi wengi wawe attention kuliko siku zote ili kujua nani atabeba kiatu ( na offcoz) kwa hili watafanikiwa sana. Safari hii watazamaji wa tuzo hizi watakua wengi kuliko kawaida.
 
Wamwombe mama awasaidie maana alishawasaidia tayari.
 
Mbumbumbu kila tournament inaruhusiwa kuweka zake unaposema zina pingana una maanisha nini?
 
UTARATIBU WA FIFA UPO KAMA IFUATAVYO.

1.Wanaangali mchezaji aliyefunga MAGOLi mengi zaidi kwenye mashindano.

2.kama wachezaji wamefungana wame( tie) MAGOLi aliyecheza MICHEZO MICHACHE ndio anapewa ufungaji Bora.

3.kama wote WAMECHEZA michezo sawa wanaangalia Mchezaji MWENYE Asisist nyingi.

KAMA TUNGEKUWA TUNAFUATA SHERIA ZA FIFA SAIDO ANGEKUWA MFUNGAJI BORA NBC 2022-2023.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…