Ndugu Dotori,
Asante kwa reference hii. Sijapata muda wa kuisoma yote, lakini niliyoyapata kwenye abstract yamenipa mwanga mkubwa tu. Kwanza kwamba tafiti zinaonesha kwamba uwezekano (probability) ya insects (sio wadudu maana kiswahili wadudu ni zaidi ya "insects") kueneza HIV ni ndogo sana. Hiyo inatia moyo sana, na ninaamini wengi watakaojipa muda kusoma ripoti hiyo watafurahi kupungukiwa na mashaka. Lakini la pili, nimeelewa kwamba probability hiyo ya kuambukizwa HIV, japo ni ndogo sana, sio zero, na kimahesabu bado hii ni muhimu (hasa katika ngazi ya individual). Kitakwimu, ni sahihi kuiacha hii, na kuelekeza nguvu za kupambana na UKIMWI katika zile njia zinazoeneza zaidi, ambazo ndio hizo zilizotajwa ngono, kujidunga masindano ya kushea nk. Kwa msingi wa hiyo article uliyoniwekea hapo (naomba uniwekee printable format kama unayo, nimeipenda sana), bado ninazo sababu (kama individual, si kama advocate wa large scale intervention) ya kuwaogopa sana mbu katika suala la UKIMWI hasa nikiwa mazingira fulani nitakayoyaeleza.
Tutumie mathematical expressions, ndizo ninazozielewa vizuri zaidi:
Let P=probability of acquiring HIV from a mosquito
P1=probability that a mosquito will be interrupted during feeding
P2=probability that a mosquito will feed on an HIV infected person
P3=probability that a mosquito will carry an infective dose in its feed
Sasa article uliyoniwekea hapo imetamka kwamba (nafupisha sasa ki-hesabu): P=P1xP2xP3
Magnitude ya overall probability (P) itategemea mambo yanayoathiri (kuongeza au kupunguza) hizo probability nyingine(P1, P2, na P3).
P1 itategemea movements zilizoko (kama feni), muwasho, watu wengine kuona ukiumwa mbu(wanamfukuza, tunafanya hivyo sana). Hizi zitatoa probabilities nyingine P1a,P1b, P1c nk. Na kwa kuwa probabilities hizi kila moja inaweza kusababisha interruption of feeding hata kama itatokea yenyewe, overall effect yake inapatikana kwa kujumlisha.
Kwa hiyo P1=P1a+P1b+P1c+.......+P1n (where n is the number of all the possible factors that can cause interruption to feeding).
P2 itategemea mambo mawili: idadi ya watu wenye HIV katika eneo husika ambalo mbu wanaweza kuhama kwa mmoja hadi mwingine, na idadi ya mbu katika hiyo "system". Probability kwamba mbu a atamuuma mtu mwenye HIV kati yetu inategemea tuko wangapi jumla, tunavyozidi kuwa wachache, probability hiyo inazidi kuwa kubwa. Probability kwamba mbu b,c,d,e nk watamuuma huyo mgonjwa ni kama hiyo ya mwanzo. Kwa hiyo probability kwamba mbu a au b au c au d nk watamuuma huyo mgonjwa ni sum ya hizo probabilities, kwa hiyo jinsi mbu wanavyozidi kuwa wengi chumbani hapo ndipo probability ya kuchukua damu ya huyo mgonjwa inayozidi kuwa kubwa.
P3 inahusu infective dose, na hii kwenye article hiyo ime-consider tu ile mbu anayobeba kwenye kile kisindano chake cha kufonzea watu.
Lakini mpaka hapa tunaona kuwa hii equation P= P1 x P2 x P3 inaanza kutisha kama mko wachache chumbani, au kama wenye HIV ni wengi (kwa mfano kwenye nursing home).
Sasa kuna moja ambalo sijalisoma kwenye hiyo article lakini huwa naliona. Huko kwetu Bongo tukiona mwenzetu anaumwa na mbu huwa tunampiga kofi yule mbu, tunafurahia anavyopasuka a kutoa damu, halafu tunashabikia "alikuwa ameshiba kweli". Halafu tuajifutafuta hiyo damu kwenye kiganja, "imetoka"! Hii ndio modification ya ile P3, volume hii ya damu ni nyingi kuliko ile ilioko kwenye kidomo cha mbu, tena ni vividly noticeable. Ukiweka hii kwenye hiyo equation, risk inazidi kuwa kubwa.
Kwa hiyo Dotori nashukuru kwa article hii, umenipa sababu ya kuendelea kuwaogopa mbu na wadudu wengine wafyonzao damu!