13. Walinda wake/waume zao.
Hili ni kundi la Me/Ke ambao muda wote wanafatana jukwaani na kugandana kama ruba.
Ukimuona mama kaanza kucomment basi jua baba yuko nyuma yake AU ukimuona baba kaanza kucomment basi jua mama yuko nyuma yake.
14. Wakeshaji wa Pm.
Hili pia ni aina ya kundi hasahasa wanaume ambao jukwaani huwaoni waki-comment, kuanzisha nyuzi, kulike au ku tag ila ukienda katika wall yao utawakuta wako active na wako online.
Kumbe wanakesha pm na u-active na u-online wao uko Pm tu.
Anatembea Pm karibu siku yake nzima kama afisa kilimo akiwa shambani
15. Wambea/wasengenyaji Pm
Hili kundi sanasana tuko sisi jinsia ya kike.
Yaani utakuta kuna umbea unatembea chini kwa chini huko Pm mpaka unajiuliza huko Pm kuna forum ingine!
Sema mambo yakitindinganya, tutajua Jf nzma.