Aina 5 za aliens wanaowasiliana na dunia

American wanavyopenda sifa naamini wangewaonyesha Aliens kwenye maonesho, walivyo tudanganya wamefika mwenzin wakatupia picture za mwenzin lakini kwa Aliens utasikia kwenye mitandao tu. Dah Aliens kwenye picture wamevaa vizuri
 
Ahsante kaka.. Huku pananifaa sana kupita maelezo
 
Yahyel waje tu niwajaribu kama wanafanana na mabinti zetu...kama wanafanan vibuti na mizinga basssss tena
 
Wakati nikiwa mdogo baba alikuwa akiniambia, ''Mwanangu nikiwa chumbani nimepumzika, akija mtu mwambie sipo". Nilifanya hivyo japo nilikuwa naumia moyoni kwa maana nilisema uongo huku nikijua kabisa kwamba baba yuko ndani amelala. Wakati mwingine alipokuwa akikaa sebuleni na mgeni kaja nilisema yupo maana niliamini akienda chumbani tu, ndipo hahitaji bughudha na ilitakiwa niseme hayupo labda awe ametoa maagizo mengine.

Pindi hayupo nyumbani nilisema kwa kujiamini kabisa kwamba hayupo (tena kwa sauti ya juu isiyo na hofu ndani yake) kwa kuwa nilikuwa na uhakika kabisa kwamba hayupo. Wakati mwingine hata kama sijamwona na sina uhakika kama yupo ndani ama la! nilikimbia chap chap hadi chumbani kwake na kuangalia kitandani kama yupo ama la! nilirudi na kusema kwa sauti ya kujiamini kabisa kwamba hayupo!

Kile kitendo cha kusema baba hayupo huku nikijua kabisa kwamba yuko ndani kilikuwa kikinisononesha, na hata namna ya kujibu kwamba hayupo ilikuwa ya kinyonge kabisa. Lakini kama kweli baba hakuwepo nilijibu kwa kujiamini sana na kwa sauti ya juu kwa kuwa tu nikikuwa na uhakika na kile ninachokisema.

Binafsi napenda sana kusema ukweli kwa kuwa ukweli humuweka mtu huru hivyo ndivyo niaminivyo mimi. Napenda sana kuuliza,kuhoji na kutafuta ukweli ama uhakika wa jambo hasa nikihisi kuna walakini katika jambo hilo. Huwa niko tayari kumaliza muda mwingi sana kufuatilia jambo moja bila kuchoka wala kukata tamaa. Ndio maana hata wakati niko mdogo nikipita uchochoroni na kuhisi harufu ya mzoga ama chochote kisicho kawaida lazima ilikuwa nifuatilie na kujua ni nini hasa kinanuka.

Msimamo wangu huo umeniponza mara kadhaa lakini pia nimefaidika sana na kujifunza mengi ikiwemo kuwa jasiri na mwenye kujiamini wakati wote. Lakini mtu anaweza kuamua kuwa mtumwa kwa kusema uongo labda kwa kutojua ama kwa makusudi. Uhakika ni jambo la msingi sana katika kushikiria misimamo yetu. Chagua kuwa huru...

Uwepo wa kitu/mtu ama nguvu inayoitwa MUNGU ni jambo ambalo sio tu haliwezekani bali halipo kabisa (according to me) na halitakuwepo. Ninaamini kwamba Mungu ni wazo la mwanadamu katika harakati zake za kutafuta asili yake. Mwanadamu anapokosa majibu ya baadhi ya mambo anayoyaona ama kuyasikia basi huhisi kwamba lazima kuna nguvu flani ipo ambayo huongoza kila kitu.

Mfano wa maswali ya mwanadamu yanayomuumba mungu ni haya;

1. Kwanini sisi (wanadamu) tuna akili (utashi) ya kutambua mambo, tofauti na wanyama labda?.
2. Kwa nini jua linatoka Mashariki kila siku na kuzama Magharibi kila siku?
3. Tunakwenda wapi baada ya kifo?
4. Kwanini tunazeeka? N.k

Huku ndiko mimi nakuita kumuumba Mungu..

Japo majibu yapo na ni marahisi sana kwa wale wanaoelewa acha wale wasiotaka kusikia kabisa maelezo hayo. Sisi wanadamu ndio tunaomuumba Mungu (idea of God) na si vinginevyo. Hoja za utetezi wa uwepo wa Mungu zimejaa maswali ambayo majibu yake huangukia katika kuamini bila
kuuliza (Dogmatism).

Nasema HAKUNA MUNGU kwa sababu nyingi sana lakini hapa nitachambua baadhi;

1. Haiwezekani Mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote, akae apange kuumba ulimwengu na viumbe vilivyomo tena kwa siku sita (huo ni udhaifu tayar). HAKIKA MUNGU WA HIVYO HAYUPO.

- Kitendo cha kuwaza kwamba nifanye hiki ama kile ni udhaifu ambao unampunguzia sifa ya kuwa unMgu mnayemuabudu. HAKIKA MUNGU WA HIVYO HAYUPO.

2. Kitendo cha Mungu mwenye kila uwezo kupata HASIRA, CHUKI, HUZUNI, GHADHABU, FURAHA ni udhaifu pia, maana nijuavyo mimi ili upate hasira huzuni na furaha lazima upate Habari mpya. Haiwezekani Mungu anayejua yajayo kupata habari mpya labda asiwe na sifa ya kujua yajayo. HAKIKA MUNGU WA HIVYO HAYUPO.

3. Mungu ambaye anaelezewa katika vitabu zaidi ya 100 huku waumini wakitofautiana kuanzia imani hadi jinsi ya kuabudu.

- Uwepo wa dini zaidi ya 100 ni ishara mojawapo kwamba mwanadamu ndiye anamuumba Mungu. Mfano ikiwa Waislamu wana Mungu wa kweli, basi ile kujilipua mbele ya umati kwa ajili ya kupigania dini yao ni sahihi mbele za huyu Mungu.

- Mungu anayeahidi zawadi Wanadamu baada ya kuua wenzao.

- Mungu anayeabudiwa kwa kafara tena ya binadamu. HAKIKA MUNGU WA HIVYO HAYUPO.

4. Mungu mwenye uwezo wote na nguvu zote lakini akashindwa kuumba ulimwengu ambao maovu hayapo. Uwezo wake uko wapi ikiwa ameumba ulimwengu uliojaa uonevu, umaskini, kafara, njaa, visasi na kila aina ya utesaji.

- Mungu anayeacha watoto zaidi ya Mil.70 wakifa kila mwaka huku wakiwa vitandani na mama zao wakimwomba Mungu awaponye lakini Mungu hafanyi hivyo labda kwa sababu hawezi kuwasaidia ama hana uwezo wa kuwasaidia.

- Mungu aliyemuumba shetani (kama yupo) kisha anashindana naye kumgombea mwanadamu. HAKIKA MUNGU WA HIVYO HAYUPO.

5. Mungu aliyeweza kumuumba mwanadamu na kumpa pumzi anayoivuta Automatically lakini alishindwa kumfanya mwanadamu amfahamu direct bila kumsoma darasani. HAKIKA MUNGU WA HIVYO HAYUPO.

6. Mungu aliyeshindwa kutafuta namna nzuri ya kuwasamehe watu makosa yao isipokuwa kuja chini sijui katika nafsi ya pili kuteswa na kisha kufa. HAKIKA MUNGU WA HIVYO HAYUPO.

- He came for himself, die for himself in order to save himself from himself!

7. Mungu anayekaa na kuhesabu makosa ya mwanadamu kisha aje amchome moto siku ya mwisho.

- Huyu Mungu si ndiye anayejua yajayo? Ana haja gani ya kuhukumu kwa kitu anachokiongoza kutokea?. HAKIKA MUNGU WA HIVYO HAYUPO.

"Dunia ama ulimwengu upo kama ulivyo, kuwepo kwa muumba ama nguvu flani hutegemea utashi wetu''. Free Ideas.

Note: There might be god but not the god of Muslims, Christians, Judaism or Budha ....

Karibuni..
 
crishna alitoka nae huko? je budha? hiyo ni uelewa wako tuu, crishna was there 4000yrs before Christ toka nje ya duara mkuu!
 
Kama sikosei umeulizwa swali hilo baada ya kusema sasa mnajua kila kitu,hayo maswali sio kwamba bali umeshajiwekea mpaka wa kufikiri kwa kudhani kila jambo itatumika sayansi.
 
Hivi wewe una umri gani?
 
Hivi viumbe uwenda vikawepo,Ngumu kuvitofautisha na Majini lkn uwenda ikawa ni majini na mashetani.....
 
Mkuu Mshana ,Mzizimkavu kuna vijitu vinaitwa vibwengo vinatofauti na allien
 
Misifa ya wazungu sasa wanajosifia kuwa na majini yao ndiyo yenye akili sana, kuliko ya ulimwenguni sifa za kijinga.

Wenzao tunajisifia kuwa Mungu wa kweli na mmoja aliye MTAKATIFU..
 
Misifa ya wazungu sasa wanajosifia kuwa na majini yao ndiyo yenye akili sana, kuliko ya ulimwenguni sifa za kijinga.

Wenzao tunajisifia kuwa Mungu wa kweli na mmoja aliye MTAKATIFU..

HAKUWEZI KUWA NA MUNGU MTAKATIFU ALIYEUMBA DUNIA ISIYO TAKATIFU.

Karibu katika ulimwengu huru

........Free ideas.........
 
Umeelewa lakini swali langu vizuri?

Enzi za ujinga watu waliweza kudanganywa kirahisi na hakuna aliyehoji.Mtu aliweza kusema ametokewa na sijui malaika kisha akapata wafuasi.Sasa hivi watu wameelimika na wanajua uongo wote.

Amka leo hii mchukue mwanao useme eti bwana mungu kakwambia ukamtoe kafara sijui sadaka ya kuteketeza(refer Abraham) ,Kwanza utapimwa akili kama iko sawa(jiulize kwa nn).kisha utafungwa kwa kujaribu kuua.

Hizi sio enzi za akina mudi kuibuka na kusema eti mungu kanichagua mimi niwe mtume wake,eti mungu akamfuata pangoni na kumuambia vitu hivo.


Karibu katika ulimwengu huru

..........Free ideas......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…