Aina gani ya choo ni bora zaidi?

Aina gani ya choo ni bora zaidi?

Joined
Feb 15, 2020
Posts
10
Reaction score
3
Habari wanajukwaa

Kumekuwa na debate zinaendelea kuhusu ubora wa vyoo hivi vya kisasa wanavyosema havijai kamwe kulinganisha na vile vilivyozoeleka.

Naomba kuuliza kwa mwenye uelewa, kipi ni choo bora zaidi kwa matumizi ya mazingira yetu ya kitanzania, hasa Dar?

Isijekuwa ni kuvutia tu biashara zao mwisho wa siku ikawa ni majuto.

Natanguliza shukrani.
 
Habari wanajukwaa.

Vilivyozoeleka ni vikoje?
 
Na hivyo visivyojaa vikoje ili tukushauri kitaalamu 😃!.
 
Acha kudanganyika, hakuna choo ambachohakijai, vyoo vyote vinajaa, kuchelewa kujaa kunatofautiana na ukubwa wa shimo tu, zingine ni mbwembwe tu, Hivyo wanavyosema vya kisasa/havijai tangu vianze hata miaka kumi bado haijafika sasa walitegemea vijae miaka mitano tu???
 
Vilivyozoeleka ni vikoje?
Mifumo Basically ipo mitatu...
1.Wenye kuhifadhi maji taka...
-Ambapo gari huja kunyonya

2.Wenye kuunganisha kwenye mfumo wa maji taka wa manispaa
-maji ya vyooni na jikoni yanapelekwa kwenye chemba za mtaa

3.Wenye Kutoreshea maji taka hapo hapo kwenye kiwanja.
-Mashimo makubwa kujengwa na yenye kuruhusu maji taka kutorekea ardhini

Ambapo katika hiyo mfumo namba mbili ndiyo bora...

Sasa hapo unalenga mfumo upi...?
 
Hapo nimelenga mfumo namba moja na tatu mkuu.
 
Nmewahi kumuulza promota wa vyoo visivojaa...nili ask simple qn?.... Mechanism gan inatumika choo kutojaa ....chaliii anasema huwa kuna BACTERIA 🦠 wana wekwa ili wawe wana kula mizigo yenu....

Nka ask at last... Bacteria huwa mnaztoa wap hajawahi kuni cheki had leo...
 
Hapo nimelenga mfumo namba moja na tatu mkuu.
Namba 1 na 3 ni kitu kimoja. Sema kuna kausanii kanafanyika kudanganya watu.

Mfumo huohuo mmoja ukiuweka Kimara na Bunju kuna sehemu moja utalazimika kunyonya majitaka na kwingine utazeeka shimo halitokaa lijae...
 
Me nakuja kuzungumzia vyoo Hivi tunavyoviita vya kisasa!

Hivyo Vyoo mnavyosema vya zamani tayari mna majibu yake kwamba vinajaa....Wait nile kitumbua kwanza nakuja!
IMG-20240321-WA0014.jpg
 
UKWELI KUHUSU MASHIMO YA KISASA

Siku hizi kumekuwa na MATANGAZO mengi sana yanayoelekeza kuhusu mashimo Haya Tunayoita Ya Kisasa YasiyO jaa!

Umeshajifunza nini kuhusu Suala hili?!?

Njoo Nikupe Ukweli sasa!

Ukweli ni kwamba Haya Mashimo YanaJaa Ila kujaa kwake Yanachukua muda mrefu sana! Makadirio ni Miaka 50 na kuendelea!

Tunasema Hayajai kwa sababu Yanachelewa kujaa! Ila kuna Namna ya Kujenga ili Yasijae! Sio kila eneo Ujenzi unalingana!

Kuna sehemu Zenye mawe mawe Au ni Pagumu kama Maeneo Ya Musoma...Tabora....Mwanza....na maeneo Mengine kama Dodoma au Hata hapa kigamboni Dsm....So ujenzi wa Kigamboni utakuwa tofauti na Chamazi na ujenzi wa Mwanza utakuwa tofauti na Mikoa ya Pwani hii Yote ni kwa sababu Ardhi zetu hazifanani!

Kuna watu wanasema Wanajenga kwa Laki 8 kila kitu kwao....na Wengine Wanasema wanajenga kwa million 1 kila kitu kwao halafu kuna mimi nasema Nahitaji Million 1.2 kwa Dsm na Mikoani nakuja Kwa million 1.4

Bei zinatofautiana kulingana na ugumu au wepesi wa kazi! Kuna shimo niliitwa kurekebisha mwanaNyamala Aliambiwa halijai ila likajaa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23] na alilipwa laki 8 alipoitwa Akaenda na akajaribu kusolve ikashindikana!

Nakukumbusha tu ukitaka vitu Vya Bei cheap ujue kabisa lazima utagharamika sana baadae! Fanya vitu kwa weredi....Kama unataka vitu vizuri andaa bajeti inayoeleweka na inayotosha!

Unataka Vyoo visivyo Jaa kwa bei Ya vyoo vya kawaida huwezi kupata! Ni vizuri kujua kwamba matofari yenye uwazi sio Suluhisho la Kujaa kwa mashimo HaYa....kuna Utaalamu wake.....

Kama unahitaji huduma hii kwa Dsm utaipata kwa Million 1.2 na mikoani utaipata kwa Million 1.4 ...Tunakuja kwa nauli zetu Popote ulipo!

Cont : 0789005562

Wasap : 0789005562
FB_IMG_1719222253900.jpg
FB_IMG_1719222258165.jpg
FB_IMG_1719222234840.jpg
FB_IMG_1705231913555.jpg
FB_IMG_1705231916402.jpg
 
Habari wanajukwaa.
Kumekuwa na debate zinaendelea kuhusu ubora wa vyoo hivi vya kisasa wanavyosema havijai kamwe kulinganisha na vile vilivyozoeleka.
Naomba kuuliza kwa mwenye uelewa, kipi ni choo bora zaidi kwa matumizi ya mazingira yetu ya kitanzania, hasa Dar?
Isijekuwa ni kuvutia tu biashara zao mwisho wa siku ikawa ni majuto.
Natanguliza shukrani.
Ukitaka choo kisijae kimwagie chumvi ya mawe hakijai milele
 
Nmewahi kumuulza promota wa vyoo visivojaa...nili ask simple qn?.... Mechanism gan inatumika choo kutojaa ....chaliii anasema huwa kuna BACTERIA 🦠 wana wekwa ili wawe wana kula mizigo yenu....

Nka ask at last... Bacteria huwa mnaztoa wap hajawahi kuni cheki had leo...
Aliyesema wanaweka bacteria yupo sawa ila hajui kinachofanyika ndo maana alishindwa. Ninatumia mfumo huo wa bacteria, na uko very effective ila uswahilini kwetu hautafanya kazi vizuri. Kwanza lazima ujue kwa usahihi volume ya shimo na kiasi cha majitaka yako, kisha kuwe na hewa ya kutosha kuruhusu aerobic respiration ( anaerobic respiration itazaa balaa), kwetu hapa tunaweka vidonge vitatu vya dormant bacteria kwenye tank la sewage lenye ujazo wa 10,000 cubic meter. Vidonge hivi huletwa tok kampuni ya Red Fox ya UK.
 
Unaijua ule msemo baba tafuta ela ili njia ya chooni isiote nyasi? Kwa taarifa yako choo Bora kile ambacho kipo mita kuanzia 50 kutoka nyumbani kwako, cha shimo na juu hajaezekwa
 
Ukishatumbukiza hawa bacteria kwenye tank, wataamka na kuanza kula ule mzigo, matokeo ya hiyo bio degradation inatoa maji na carbon dioxide, CO2 itaenda angani na maji yataishia kwenye mitaro ya jiji, kabla hujaruhusu maji kuingia mtaroni, sharti uweke chlorine kali ili kuua bacteria wote waliomo ktk maji yanayoingia kwenye mtaro wa jiji. Njia hapa utakuwa umetumia aerobic system.
 
Back
Top Bottom