Aina mbalimbali za mbu na tabia zao

Aina mbalimbali za mbu na tabia zao

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
25,190
Reaction score
27,434
Mbu kiswaswadu
Huyu ni mbu msumbufu sana mara nyingi huwa hawahangaiki saaaana na damu ila wao ni kukukera tuu,yaani anakuja kama amekosea njia hivi atakupiga kumbo huku sikioni au puani alafu yeye huyooo anatimka anakuacha wewe unajimamanyua bonge la kofi kama zoba vile. Aina hii ya hawa mbua mara nyingi wanapatikana mkesha wa msibani.

Mbu changudoa
Yaani huyu mchana kweupe hata kama jua linawaka vipi yeye yupo na atakuja atalamba damu na kusepa.huyu mara nyingi anapatikana mashambani au sehemu yenye utulivu na muonekano wake ni mweupe mistari na weusi (kama pundamilia) na ni msafi balaa.

Mbu liwalo na liwe
Huyu ni wa rangi ya kaki yaani yeye hata uwe mkali vipi atakunywa damu tuu labda umuue na ni mbishi ukimfukuza anatoka hapo anahamia pembeni kidogo yaani hatimki hadi anywe damu. Na huyu pale alipokuuma panawasha sana na kuota li lenge lenge la maji.hawa mara nyingi wako kila sehemu sio mchana sio usiku.

Mbu utajua hujui
Huyu akija yeye ni kimya kimya anapiga pafu moja la maana ule mda wewe umeshtuka yeye kashajaza tank nduki unabaki unajilaumu tuu.

Mbu seng*
Yaani huyu kazi yake ni kukukera tuu yaani hatui kwenye mwili wako ila akipita karibu na wewe anatoa mlio mkali kama (miling mashine)au crosing mashine)ile mashine ya kuchonga vyuma. Hawa utasikia mlio wao tuu ila kila ukitaka hata kumwona humwoni unaambulia mlio tu.

Na hawa wote wanapatikana hapa tanzania!je!huko kwa wenzetu wapo?
 
Kuna mbu aluwatani umemsahau hapo[emoji16][emoji16]

Huyu anajiamini sana hana woga yeye popote kwenye mwili anatua na anapenda sana kunyonya zile sehemu za shoo kama usoni begani na hata kwenye msuli wa mkono.na huyu kule kote ankopiga asbh unakuta kuna mapelemaple[emoji13][emoji13]
 
Huyu anajiamini sana hana woga yeye popote kwenye mwili anatua na anapenda sana kunyonya zile sehemu za shoo kama usoni begani na hata kwenye msuli wa mkono.na huyu kule kote ankopiga asbh unakuta kuna mapelemaple[emoji13][emoji13]
😁😁😁 ana hatari uyo
 
Back
Top Bottom