Siku hizi kuna hali ambayo nimeibuka na kushika kasi mara mwanamke anapopata mimba , kama alikua hajavalishwa pete anavalishwa pete na kinachofatia ni kutangaza ndoa, imekua ni kawaida kwa bibi harusi kufunga ndoa akiwa na mimba ya miezi sita wakati mwingine mpaka nane . nimeshuhudia harusi zaidi ya tano ambazo mabibi harusi walikua na mimba . kwa wataalamu wa maswala ya dini inaruhusiwa kwa mwanamke aliye mimba kufunga ndoa, je wachungaji wanaowafungisha ndoa hiyo huwa wanafuata maadili na imani za makanisa yao.