Aina mpya ya ufungaji wa ndoa yaanza kushika kasi makanisani.

Aina mpya ya ufungaji wa ndoa yaanza kushika kasi makanisani.

CANCER

Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
36
Reaction score
20
Siku hizi kuna hali ambayo nimeibuka na kushika kasi mara mwanamke anapopata mimba , kama alikua hajavalishwa pete anavalishwa pete na kinachofatia ni kutangaza ndoa, imekua ni kawaida kwa bibi harusi kufunga ndoa akiwa na mimba ya miezi sita wakati mwingine mpaka nane . nimeshuhudia harusi zaidi ya tano ambazo mabibi harusi walikua na mimba . kwa wataalamu wa maswala ya dini inaruhusiwa kwa mwanamke aliye mimba kufunga ndoa, je wachungaji wanaowafungisha ndoa hiyo huwa wanafuata maadili na imani za makanisa yao.
 
kweli kabisa mkuu, hii kitu imeshika kasi sana yaan cku hz imekuwa kama vile ni fashion kufunga ndoa ukiwa mjazito, nakumbuka last year nlihudhuria harusi moja yaan bb harus alikuwa na tumbo kule, hakuwa comfortable hata kidogo make up zenyewe zilidunda,baada ya ndoa hakumaliza hata mwez akajifungua,,,,,

Kwa baadh ya watu ambao nimewah kuongea nao ni kuwa cku hz mambo yamebadilika vijana wanaanza ngono mapema, utoaji wa mimba nao umesababisha kwa kias kikubwa wadada wengi kuharibiwa au kutolewa vizaz, so wakaka wa siku, baadh yao sio wote wanahakikisha kuwa wapenz wao wana uwezo wa kubeba mimba ndio hatua za uchumba na ndoa kufuata.

asante
 
Siku hizi ukitaka kuolewa sharti upate mimba kwanza..Mmh..Wenzangu na mie wenye vizazi vya mbali utahangaika kuisaka mimba mpaka ukome, maana mwanaume anasubiri mimba ishike ndio atangaze ndoa.. Patamu hapo! Utaishia kuwachangia mashost zako harusi mpaka unachanganyikiwa... Wewe harusi IMEBUMA KISA?? MIMBA HAIKAMATI..Loh.. Mungu tunusuru..
 
Mchungaji hapimi mimba! Wala hana uwezo wa kuweka hicho kipengele, je kuzaa kwanza na kwenda kufunga ndoa kunaruhusiwa? Kama ndio kuna ubaya gani kuwa nayo, si sawa tuu kwenda na mwanao kanisani siku ya harusi yako.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Whether mchungaji kuchunguza mimba au kutochunguza hiyo si kazi yake. Mungu ndiye anayejua ndoa halali na ya kudumu na vinginevyo. Wanangu mambo yamebadilika. Kila zama ina kitabu chake. Ucha Mungu wa siku hizi si kama wa zamani. Ingawa haikubaliki kuanza kuojana kabla ya kufunga ndoa, kwa vile ndoa ni makubaliano ya wawili, watakavyoamua sawa. Maana ni watu wazima wenye akili timamu.
 
binaadam tumepotea sana na wala hatujuwi kama tumepotea. ili haya kukoma cha "1" turudi kwa mungu "2" utowaji wa mimba ovyo kuachwa mara 1. na wanaume kuwa na elimu juu ya mambo ya uzazi. maana unaweza kumjuwa mtu kama ana uzazi au laa kabla ya ndowa.
 
Back
Top Bottom