Aina mpya ya ushirikina

Aina mpya ya ushirikina

Ngoja niende ili nipate mchongo wa sensa
 
Huyo anayejiita Nabii ni wazi kabisa kuwa ni mshirikina.
Mtawatambua kwa matendo yao.

Inaagiza Kucha, Nywele za Biadamu alafu zifungwe kwenye kitambaa cheupe alafu ziletwe ktk Kanisa la lako ili iweje ?

Sasa hivi jina siyo kitu. Kuna Kanisa la Kristo na Kanisa la kishirikina kwa mfano Freemasoni wana kanisa na biblia yao pia.
Mkisikia Kanisa au Nabii au Mtume lazima muyapime.

Kanisa la Kristo lazima liige maagizo ya Kristo mwenyewe.


Mathayo 11:29
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

Kuitisha viungo vya Binadamu kanisani tena vifungwe ktk kitambaa cheupe na sio rangi nyingine hayo huyo Nabii wa Uwongo kajifunza kwa nani ?

Toka dunia iumbwe huyo ndio mjinga wa kwanza kumsikia akiagiza viungo vya Binadamu vifungwe ktk kitambaa cheupe na kupelekwa kanisani.

Nanyinyi waumini mna akili za namna gani.
Mtu anajitambulisha wazi kabisa kuwa ni Mchawi na munamuamini tu au hadi muagizwe kutoa kafara watoto wenu ?

Mnakuwa kama mmerogwa vile maana akili zote mmemkabidhi yeye.

Mkiona mtu kavaa suti tu basi ni Nabii.
Kweli njia ile ni nyembamba.
 
Back
Top Bottom