Aina mpya ya virusi hatari vyagundulika

Aina mpya ya virusi hatari vyagundulika

babumapunda

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
4,643
Reaction score
3,301
Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema inaelekea sana kuwa aina mpya ya virusi vinavouwa, vya coronavirus, vinaweza kuambukizwa baina ya watu walio karibu sana.

Virusi hivyo ni sawa na vile vya homa ya SARS (Severe Acute Respiratory Syndrome) na vinamfanya mgonjwa kuwa na shida sana ya kuvuta pumzi. Nchini Ufaransa mwanamume mwengine hivi sasa ni mahtuti baada ya kuambukizwa na mgonjwa wa mwanzo nchini humo, ambaye walilazwa chumba kimoja hospitali.

Hadi sasa watu 34 wanajulikana kupata ugonjwa huo duniani tangu mwaka wa 2012, 18 kati yao walikufa Saudi Arabia. WHO nasema ni muhimu kujulisha watu kuhusu virusi hivyo kwa sababu kuna wasi-wasi mkubwa kuwa vinaweza kusambaa.

Source:ITV
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1368423016435.jpg
    uploadfromtaptalk1368423016435.jpg
    7.2 KB · Views: 625
Kila siku matatizo yanazidi badala ya kupungua.nimeamin maasi ndio yanayoleta yote haya.
 
tutakoma tu maana tuanamuasi Mungu kwa kujifanya sisi sdio sisi kumbe ndio tunajiua bila kujua
 
mnh kazi ipo kwelikweli tutafika kweli yanaanzaga iv iv........taratibuuuuuuuu
 
Kila siku matatizo yanazidi badala ya kupungua.nimeamin maasi ndio yanayoleta yote haya.

Kuna virusi tayari vipo Tz, ukivipata KINGA yako inachanganyikiwa, badala ya kupambana na virusi inapambana na viungo vyako mwenyewe. kwa hiyo viungo vyote vinaanza Kuugua.
 
Back
Top Bottom