Aina na viwango vya kodi ya biashara

Aina na viwango vya kodi ya biashara

Benittotz

Member
Joined
May 24, 2018
Posts
68
Reaction score
123
ZIFAHAMU AINA ZA KODI NA VIWANGO VYAKE KWA MFANYABIASHARA
MDOGO NA WA KATI.

[emoji1006]: KODI NI NINI?

 Kodi ni mchango wa lazima kwa serikali kutoka katika malipo ya mishahara,
utoaji wa huduma au uuzwaji wa bidhaaa, gharama za nyongeza katika
kuhamisha mizigo au kiwango Fulani kinachokatwa katika miamala.
 Kodi ya biasha hutokana na mauzo ya mwaka au faida kulingana na ukubwa na
Aina ya BIASHARA.
 Serikali inahitaji Kodi katika kutekeleza miradi ya kijamii na kuleta
Maendeleo vile vile.
 Kunahitajika uwazi, usawa, gharama ndogo za ukusanyaki kodi na uchache wa
Kodi hizi ili kuleta Maendeleo chanya katika jamii husika.

AINA ZA KODI ZA BIASHARA

 Presumptive tax. Kodi ya makisio hi NI kwa wafanyabiashara wadogo wasio na
daftari za hesabu za fedha. Muhusika hutozwa Kodi kulingana na mauzo yake
ya mwaka ( annual turnover).
 Audited ta. Hi ni Aina ya kodi inayohusisha wafanyabiashara biashara wenye
vitabu vya kumbukumbu za hesabu bazo hutumika kutoa tathmini ya kiwango
cha kodi kinachopaswa kulipwa.

VIGEZO VYA KUZINGATIA KATIKA KODI YA
MAKISIO

 Mhusika anapaswa kuwa mkazi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Katika
upande wa Kodi ulikuwa mkazi vitu vitatu huzingatiwa zaidi

1. Lazima uwe na sehemu ya kumudu ya kuishi Na uwepo nchini katika mwaka
husika wa fedha. Hapa hawamaanish lazima uwe umejenga. Sehemu ya
kudumu ya makazi ni sehemu yoyote unayoishi Kama vile nyumba ya kupanda
au chumba katika nyumba ya wageni ila TU wahusika wa eneo husika wawe
wanatambua uwepo wako.

2. Uwe umeishi nchini kwa kipindi cha zaidi ya siku 183 au Zaid katika mwaka
husika wa fedha.

3. Uwe nchini katika huo mwaka wa fedha na uwe na wastani wa kuishi nchini
kwa siku zaidi ya 122 kwa kipindi Cha miaka miwili iliyopita

4. Uwe mfanyazi au afisa was serikali uliyeko nje kikazi wakati was mwaka wa
fedha.

 Biashara yako iwe inaingiza chini ya Tsh 20 million kwa mwaka.
 Kipato chote kinapaswa kutokana na biashara katika mwaka husika wa fedha.
Hivyo mhusika hapaswi kujihusisha na shughuli zinginezo kama vile ajira na
uwekezaji.
 Mapato yake ya mwaka wa fedha yanapaswa kutokana na biashara ambazo
vyanzo vyak viko ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania pekee.

VIWANGO VYA KODI KATIKA MFUMO WA
MAKADIRIO

 Katika mfumo huu kiwango Cha Kodi kinachohitajika hupatikana kwa kuzingatia mauzo ya mwaka yatakayoonyeshwa katika taarifa ya
mfanya biashara. Kama taarifa hizo hasijakamilika , makadirio mazuri hufanyika na kamishina na kiwango sahihi kupatikana..
 Viwango hivyo kwa taarifa Kamili na zisizo Kamilika vimeonyeshwa Hapo chini Kama ifuatavyo.

mapato ya mwaka
Yakiwa chini ya 4,000,000.
Makadirio ya Kodi taarifa zikiwa nusu ni;
NIL (-)
Makadirio ya Kodi taarifa zikiwa Kamili ni;
NIL (-)
Mapato ya mwaka yakiwa zaidi ya 4,000,000 lakini ni sawa auchini ya 7,500,000.
Makadirio ya Kodi taarifa zikiwa nusu ni
TSH 150,000.
Makadirio ya Kodi taarifa zikiwa Kamili ni
3% ya kiwango kilichozidi katika 4,000,000
Mapato ya mwaka .
Kiwango kinapozidi 7,500,000 lakini NI sawa au chini ya 11,500,000.
Makadirio ya Kodi taarifa zikiwa nusu ni
TSH 318,000
Makadirio ya Kodi taarifa zikiwa Kamili ni
Tsh 135,000 +3.8% ya kiwango Cha mapato kilichozidi katika 7,500,000.
Mapato ya mwaka
Kiwango kinapozidi 11,500,000 lakini Sawa au chini ya 16,000,000.
Makadirio ya Kodi taarifa zikiwa nusu ni
Tsh 546,000.
Makadirio ya Kodi taarifa zikiwa Kamili ni
Tsh 285,000 + 4.5% ya kiwango kilichozidi katika 11,500,000.
Mapato ya mwaka
Yanapokuwa zaidi ya 16,000,000 lakini sawa au chini ya 20,000,000.
Makadirio ya Kodi taarifa zikiwa nusu ni
Tsh 862,
Makadirio ya Kodi taarifa zikiwa Kamili ni
Tsh 487,000 +5.3% ya kiwango kilichozidi katika 16,000,000.

KODI YA BIASHARA KWA MFANYABIASHARA
ANAETUNZA TAARIFA ZA FEDHA

 Kundi hili hulipa Kodi kutokana na faida wanatoipata .
 Mapato ya mwaka yanazidi Tsh20,000,000.
 Hulazimika kuandaa taarifa ya fedha ya mwaka.
Mchanganuo was Kodi upo Kama ifuatavyo;

UPANDE WA TANZANIA BARA.

Kiwango kinachopaswa kutozwa Kodi kwa mwaka
Mapato ya mwaka yasipozidi 20,400,000.
Hakuna Kodi (-) NIL
Mapato yanapozidi 20,400,000 lakini yakawa sawa au chini ya 4,320,000.
Kiwango Cha Kodi mi 9% ya ziadi iliyozidi katika 20,400,000.
Mapato yanapozidi 4,320,000 lakini yakawa sawa au chini ya 6,480,000.
Kiwango Cha Kodi ni 205,200 + 20% ya kiwango kilichozidi katika 4,320,000.
Mapato yanapozidi 6,480,000 lakini yakawa sawa au chini ya 8,640,000
Kiwango Cha Kodi ni 637,200 +25% ya kiwango kilichozidi katika 6,480,000.
Mapato yanapozidi 8,640,000
Kiwango Cha Kodi ni 1,177,200 + 30% ya kiwango kilichozidi katika 8,640,000.

UPANDE WA ZANZIBAR

Mapato ya mwaka yasipozidi 1,800,000.
Kiwango Cha Kodi ni Hakuna (-) NIL
Mapato yakiwa zaidi ya 1,800,000 lakini chini au sawa na 4,320,000.
Kiwango Cha Kodi ni 13% ya kiwango kilichozidi katika 4,320,000.
Mapato yakiwa zaidi ya 4,320,000 lakini chini au sawa na 6,480,000.
Kiwango Cha Kodi ni 327,600 +20% ya kiwango kilichozidi katika 432,000.
Mapato yakiwa zaidi ya 6,480,000 lakini chini au sawa na 8,640,000
Kiwango Cha Kodi ni 759,600 + 25% ya kiwango kilichozidi katika 6,480,000.
Mapato yakiwa zaidi ya 8,640,000.
Kiwango Cha Kodi ni 1,299,600 + 30% ya kiwango kilichozidi katika 8,640,000.

HITIMISHO

 Ni imani yangu katika makala hii fupi umepata mwangaza kiasi fulani katika maswala ya Kodi hususani
katika biashara ndogo ndogo.
 Nakaribisha maoni, nyongeza na marekebisho pale ambapo Kuna kitu umeona taarifa Yale haiko sawa.
 Tukutane katika makala zijazo .

IMEANDALIWA NA

BENSON FLEXON SHIRIMA
MHITIMU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM SHULE YA BIASHARA .
MWANZILISHI NA MMILIKI WA @CHIKAZI_POINT
EMAIL : bensonflexon@gmail.com
FACEBOOK BENSON FLEXON SHIRIMA
INSTAGRAM @BENITTO_TZ
WATSAP 0654859954
CALL/TXT 0653384656
 
ZIFAHAMU AINA ZA KODI NA VIWANGO VYAKE KWA MFANYABIASHARA
MDOGO NA WA KATI.

 Viwango hivyo kwa taarifa Kamili na zisizo Kamilika vimeonyeshwa Hapo chini Kama ifuatavyo.

mapato ya mwaka
Yakiwa chini ya 4,000,000.
Makadirio ya Kodi taarifa zikiwa nusu ni;
NIL (-)
Makadirio ya Kodi taarifa zikiwa Kamili ni;
NIL (-)
Mapato ya mwaka yakiwa zaidi ya 4,000,000 lakini ni sawa auchini ya 7,500,000.
Makadirio ya Kodi taarifa zikiwa nusu ni
TSH 150,000.
Makadirio ya Kodi taarifa zikiwa Kamili
 
inakuaje mtu mtaji 2m adi 4m afu mapato anapangiwa laki5,
Au cjaelwa vzur..
Hapana mkuu, kinachoangaliwa katika mtaji mdogo ni mauzo yako ya mwaka,Kama jumla ya mauzo yako hayafiki 4m hulipi Kodi, itakapotokea imezidi ndio unalipa kulingana na kiasi kilichozidi
 
Hapana mkuu, kinachoangaliwa katika mtaji mdogo ni mauzo yako ya mwaka,Kama jumla ya mauzo yako hayafiki 4m hulipi Kodi, itakapotokea imezidi ndio unalipa kulingana na kiasi kilichozidi
apo sawa,
Na jeinakuaje pale mtu unaenda omba leseni yabiashara TRA, afu ndo una anza biashara ila wao wana kukadilia 360 kwa mwaka??
 
apo sawa,
Na jeinakuaje pale mtu unaenda omba leseni yabiashara TRA, afu ndo una anza biashara ila wao wana kukadilia 360 kwa mwaka??
Unakadiriwa kwa kuwa taarifa hasijakamilika, na wanakukadiria kulingana na ukivyojaza fomu yako. Ila utakapofanya biashara mwaka mzma na mauzo yako yasifike 4m bas una haki ya kuandikaa maombi kwa kamishna na utakuwa hulipi Kodi .. ila itakapozidi bas inabd kwaku dai Kodi kulingana na asilima za kiwango kilichozidi katika 4m mf. Mauzo yako ya mwaka yakiwa ni 6 m kiwango kilichozidi Hapo ni 2m hivyo wataichaji hiyo 2m kulingana na % zinazostahili kisheria
 
Sasa inakuwaje kwenye application za huo ufafanuzi unakuwa vingine ?? Kwanini watu wanafunga biashara zao, kwanini watu wanahamisha biashara zao nchi jirani kwa sababu ya unafuu wa kodi wakati kwa mitaji yao ilitakiwa walipe kodi ndogo zaidi kuliko wanavokadiriwa.

Tatizo lipo wapi
 
ili ulipe kodi inatakiwa mauzo yawe kuanzia 10 million na kuendelea kwa mwaka na siyo million 4
 
Hapo kwenye kukadiriwa na elimu ya Kodi ndipo penye tatzo Kubwa zaidi. Kama unafahamu taratibuu zote NI rahisi kukadiriwa kiwango sahihi, wanaohamisha biashara nje Hawa NI WAFANYABIASH wakubwa,Kodi zao hazikadiriwi. Zinalipwa kulingana na faida wanayoonyesha kwenye taarifa ya mwaka wa fedha
 
ili ulipe kodi inatakiwa mauzo yawe kuanzia 10 million na kuendelea kwa mwaka na siyo million 4
Kodi ya Aina ipi hapa tunamzungumzia? Presumptive tax au audited tax? Manake kwa mwongozo wa Income tax act 2004 ni 4m annual turnover
 
Hapo kwenye kukadiriwa na elimu ya Kodi ndipo penye tatzo Kubwa zaidi. Kama unafahamu taratibuu zote NI rahisi kukadiriwa kiwango sahihi, wanaohamisha biashara nje Hawa NI WAFANYABIASH wakubwa,Kodi zao hazikadiriwi. Zinalipwa kulingana na faida wanayoonyesha kwenye taarifa ya mwaka wa fedha

Ok kama ulifatilia mwezi uliopita Wafanyabiashara wengi pale Tunduma walihamishia biashara zao Zambia. Mkuu wa Mkoa wa Songwe aliwaendea kwa lengo la kuzungumza nao warudishe biashara zao Tanzania na akaahidi kuwapatia ufumbuzi juu ya suala la kodi, lakini mpaka leo imeshindikana. Sasa Zambia wamewezaje kuweka mfumo mzuri wa kodi ulio rafiki kwa wafanyabiashara hasa hawa wadogo wadogo ?
 
kitengo cha elimu TRA hakifanyi kazi inavyotakiwa, walipa kodi wengi hawapewi elimu kama hii, hawajui kwa mtaji kiwango fulani, kodi ipi unatakiwa kulipa kwa wakati gani.

nyinyi TRA kitengo cha elimu tokeni ofisini mfunze watu, siyo vibaya mumuajiri na huyu kijana awasaidie hiyo kazi.
 
Wamekaa tu na masura yao utadhani sijui wadudu gani wanasubiria mshahara ambao hawautendei haki hata kidogo.....wanaboa sana kwakweli
 
Unakadiriwa kwa kuwa taarifa hasijakamilika, na wanakukadiria kulingana na ukivyojaza fomu yako. Ila utakapofanya biashara mwaka mzma na mauzo yako yasifike 4m bas una haki ya kuandikaa maombi kwa kamishna na utakuwa hulipi Kodi .. ila itakapozidi bas inabd kwaku dai Kodi kulingana na asilima za kiwango kilichozidi katika 4m mf. Mauzo yako ya mwaka yakiwa ni 6 m kiwango kilichozidi Hapo ni 2m hivyo wataichaji hiyo 2m kulingana na % zinazostahili kisheria
Taarifa kukamilika ni kwa kiwango gani maana unaulizwa maswali yote na kuyajibu km mauzo kwa siku ambayo wao ndio hukadiria kwa mwaka,mkataba wa pango,km una familia,umemuajiri mtu au upo mwenyewe ktk hiyo biashara au ni taarifa zipi hizo ambazo ukitoa unaepuka kulipa kodi km mauzo yako kwa mwaka hayafiki 4m
 
Back
Top Bottom