lucky sabasaba
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 1,656
- 1,204
Kuwait dinar ndiyo pesa yenye nguvu kuliko zote kwa sasa ambapo ukiwa nayo moja ni sawa na hii yetu(Tsh 5509)..ya pili ni Bahrain dinar ambayo moja ni sawa na TSH 4169..Ya tatu ni Oman rial ambayo moja ni sawa na Tsh 4067 ya nne ni latvia lats ambayo moja ni Tsh 2921 na ya tano ni Uk Pound ambayo moja ni Tsh 2409 japokuwa zina badilikabadilika lakini hizi ndio pesa zenye nguvu sana,kwa mpangilio huu dola ni ya kumi na tatu katika pesa zenye nguvu,kuna bwana mmoja aliniambia pesa ya mwarabu ina nguvu kwa ajiri ya mafuta inawezakuwa kweli lakini ni kwanini Nigeria ambayo ni ya sita duniani kwa uzalishaji wa mafuta pesa yao (Naira)haina nguvu??maana pesa ya kenya ina nguvu kuliko ya nigeria..ni vitu gani vinavyofanya pesa ya nchi iwe na thamani???niliambiwa kuna kipindi cha nyuma 1960s pesa yetu ya tanzania ilikuwa na nguvu sana tsh moja ilikuwa kama dola 5 na ilikuwa na nguvu kuliko ile ya kenya,sasa inaporomoka kila siku us dola moja ni sawa na shilingi ya kwetu 1600 wakati us dola moja ni shilingi kama 80 za kenya!!!kwa afrika pesa nne zilizo na nguvu ni cedi ya ghana..pound ya sudan..botswana pula..na rand ya SA...au ufisadi pia unachangia pesa kushuka??maana nigeria kama nilivyosema ni ya sita duniani katika kuzalisha mafuta..inazalisha mafuta mara kumi zaidi ya nchi ya UAE lakini pesa yake naira haina nguvu sana..kwa nini???