Aina ya biashara ambayo unaweza kuanzisha chuoni

Aina ya biashara ambayo unaweza kuanzisha chuoni

Msaada ni aina gani ya biashara nayo weza kuanzisha chuoni na ikanipa faida.
Kuna uzi upo huku umejibu swali lako ukikosa nenda ka google alafu uchangue yenye link ya Jf. Au zingatia wazo la huyu mkuu
Uza nguo za kiume. Boksa, vest, jezi kadeti.
kwa kuboresha tu labda awe na kasimple site (website) kwa ajili ya kuweka bidhaa zake mtu akiipenda anampigia direct
'mm pia na project inafanya (na-code systeam) kwa ajili ya wanafunzi kupiga ele wakiwa chuo
 
Kama ni wa kike basi jifunze kufanya make up kwa akina dada, maana chuoni unajua tena kuna mitoko mingi kila weekend, kuna wakati kuna party za birthday kuna zile za faculty au za professional yenu, wakati mwingine baby shower maana chuo wadada kuwa wajawazito ni swala la kawaida, naamini unaweza jiingizia kipato kupitia hiyo huduma ya make up na inaweza kuwa mobile wewe ndio unawafuata kwenye hostel zao.
 
Kuuza nguo, culture za kimasai za viatu , bangili. Vocha na uwe na printer machine.
Hii utakuwa unaprint assignment maana kuna wakati uhitaji wa kuprint unakuwa juu sana huku printer za chuo zikiwa chache.
 
Msaada ni aina gani ya biashara nayo weza kuanzisha chuoni na ikanipa faida.
Mimi nilikua nafanya biashara ya kuuza diary nilikua naenda kariakoo nanunua diary zilizo pita muda wake kwa jumla nilikua napata kwa 2000 au 2500 ninaenda kuzaa 3500 ad 4000 wanafunz wengi wa chuo wanapenda kutumia wakat wa kutake note
 
Msaada ni aina gani ya biashara nayo weza kuanzisha chuoni na ikanipa faida.
Kama uko serious na masomo na hutaki kufeli, biashara rahisi kuicontrol ni ya kuuza vocha,mpesa/tigopesa,na kuprint/photocopy documents.
Hizi ndio utaweza kuzimudu bila stress yoyote yaani unakaa tu hostel unasoma notes huku unasubiria wateja.
 
kukopesha pesa,kama una PC fanya typing unachapa kazi za watu(hizi nilifanya nikiwa chuoni UDSM),weka kibanda cha chips,tandika chini uuze mitumba mikali ya kijanja mfano suruali na mashati. baadhi ya biashara zinahitaji uwe na mtu wa kusimamia.
 
Back
Top Bottom