Aina ya Mazoezi yanayofanya Tumbo zuri bila ya kuwa na mtaalamu wa mazoezi ya kiuno

Aina ya Mazoezi yanayofanya Tumbo zuri bila ya kuwa na mtaalamu wa mazoezi ya kiuno

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Ni kitu kisichopingika kuwa mtu kuwa na muonekano mzuri anahitaji kuwa na umbo zuri pia. Wanawake hasa waliozaa huwa na matumbo makubwa yanayoharibu muonekano wao mzuri. Mazoezi haya yatakusaidia kuwa na tumbo zuri (Flat belly).

Aina ya Mazoezi Yanayofanya Tumbo Zuri Bila ya Kuwa na Mtaalamu wa Mazoezi ya Kiuno (Waist Trainer):

Bicycle crunch ~> Lala chali huku mikono yako ikiwa nyuma ya kichwa, kunja magoti yako nyuzi 90 halafu fanya kiwiko cha kulia kikutane na goti la kushoto. Badili kila upande.

DQsx-_UWkAAxM4G.jpg


Triangle crunch ~> Piga magoti huku mguu wako wa kulia ukiwa umeunyoosha, Weka mkono wa kushoto chini, mkono wa kulia nyuma ya kichwa. Leta goti la kulia kwenye kiwiko cha kulia.

DQsxMnyWkAEyke4.jpg


V-ups or knee hugs ~> Lala chali, nyoosha miguu na mikono yako, Jaribu kukutanisha miguu na mikono yako juu ya kiuno chako. Fanya hivyo walau mara 15.

DQsw0O-W0AAIXC4.jpg


Jack knife ~> Lala chali ikiwa ni pamoja na kunyooya mikono yako. Kuanzia hapo sogeza mkono wako wa kulia kushika mguu wa kushoto. Fanya hivyo pande zote walau mara 15.

DQsvbi7X4AI8rYB.jpg


Heel grabbers ~> Lala chali huku mikono ikiwa chini pia, inua kifua chako huku ukijaribu kushika visigino vyako kwa kila upande mara 15.

DQst2ZAX0AExokG.jpg


Side plank with twist ~> Lala ubavu, weka mkono wako mmoja nyuma ya kichwa kisha fanya kama unajaribu kuleta kiwiko chako chini. Fanya hivyo walau mara 15 kwa kila upande.

DQsr8yOUEAAHgwD.jpg
 
Somo zuri.

Na kwa kupungua mwili mzima nahitaji mazoezi ya namna gani?
 
Back
Top Bottom