SankaraBoukaka
JF-Expert Member
- Jul 2, 2019
- 1,213
- 1,918
Simba kama moja ya klabu kubwa Afrika inahitaji kuwa na wachezaji wenye mwendelezo mzuri wa perfomance kiwanjani ili idumu kwenye hadhi na nafasi yake.
Tokea msimu huu 2021/22 umeanza imeonekana kwamba Kibu Denis na Bernard Morrison wameingia kwenye kikosi cha kwanza. Ni wachezaji wazuri sana kwenye kasi na mara nyingi husababisha faulo nyingi kutokana na hiyo kasi yao.. Na wamefunga na magoli muhimu kwenye mechi walizocheza.
Tatizo walilonalo hawa wachezaji ni ubinafsi uliopitiliza ambao unainyima Simba nafasi ya kufunga magoli mengi kwenye nafasi zilizo wazi.
Hawa wachezaji wanapenda ku-dribble, yaani wao kila muda ni kukaa na mpira sana miguuni wakati wenzao wameshaji-position vizuri kiufungaji au kuelekea kwenye goli pinzani. Ujinga zaidi mwishowe hupoteza kizembe au hulazimisha kupiga mashuti yasiyo na madhara yoyote kwa timu pinzani.
Mechi na JKT Tanzania kijana Mwinuke alifanya mambo ambayo Kibu Denis ni nadra au hayawezi kabisa kufanya, nafkiri kama angeamainiwa basi angkuwa na msaada kuliko Kibu ambaye ni JESHI LA MTU MMOJA.
Mpira wa kisasa unahitaji wachezaji wanaocheza kitimu, kwakuwa ndo mfumo wenye manufaa zaidi kuliko uchezaji wa kibinafsi usio na manufaa.