Mi timu yetu ya simba huwa naiona kama haina makocha vile, kwanini nasema hivyo.
System ya wachezaji haijawahi kubadilika yani mchezaji anakua na makosa yale yale msimu mzima kwa mfano Wawa huwa ni mzembe wa kuruka kapombe anapiga cross za hovyo kibu anapenda kukimbia tu hataki kutoa pasi, morrison anacheza kama vile timu ya babake.
Sa najiuliza huko mazoezini makocha huwa wanafanya kazi gani? N kama ni wachezaji hawafundishiki kwanini wasipigwe sub au wakaachwa kabisa.
Morrison ni mchezaji mzuri akiachana na show off, alikadhalika kibu
Kibu ni kijamaa fulani hivi chenye ubinafsi na choyo, hua nakivutia picha sijui kinaishije huko mtaani hawa ndo type ya wale watu wanaonyima hata maji ya kunywa ukiomba