Kibenje KK
JF-Expert Member
- May 28, 2016
- 270
- 391
Kuna watu wako maalum KUUA NDOTO YAKO(Dream killer) , Ni aina ya watu wabaya ambao kazi yao ni kuhakikisha wewe hufanyi kitu na hufanikiwi kutimiza ndoto yako.
-
Ni watu gani?
-
1.Mtu mwenye imani ndogo.
Huyu ni mtu anaamini katika udogo, haamini kama unaweza kuwa na biashara kubwa, haamini kama unaweza kufika mbali, haamini kama unaweza kujisimamia mwenyewe ukafika mbali.
( Atakuambia haiwezekani kwenye kila jambo kubwa unalolitaka)
2.Mtu mwenye Wivu mbaya.
Hawa ni watu ata ukinunua gari wataanza '' Gari yenyewe ina rangi mbaya na hizi ajali za siku hizi''
Watasema ''Duh umeona mwanaume aliyeolewa naye? Ndo mwanaume gani?
Hawa hata ufanye zuri la namna gani, kwa sababu ya wivu wao hawawezi kukusifia sana sana watakukatisha tamaa uwe kama wao. (mafanikio yako yanamuhuzunisha) ndo wale nguo nzuri ila shape yako sasa 🤣🤣
__
3.Mtu aliyeumizwa sana na ambaye moyo wake haujapona vizuri. Huyu atakushauri kwa hasira na uchungu. Mara nyingi hawa wako kwenye mahusiano. Atakwambia wanaume wote ni ...., hakuna mwanamke wa kuoa siku hizi, biashara hazilipi, hakuna kazi za maana.
Hawa yaliyowatokea kwao hudhani ni lazima yatokee kwako pia.
_____
4.Mtu anayekukosoa-kosoa.
Hawa wamejaa sana, Binafsi mwanzoni nilikutana nao sana, hawa dawa yao ni kuziba masikio huwa hawaoni lolote jema. wakati mwingine sikiliza na jirekebishe inapobidi lakini nia yao ni kukufanya ujione hujui kitu.
_
5.Mtu asiye na Maono.
Kipofu wa kifikra, Huyu hana ndoto inayomsukuma kufanya kitu, Ni aina ya watu waliokuja Duniani kutembea yaani chochote kinachotokea anaona ni sawa tu. Huyu ukiwa karibu naye atakuharibia ndoto yako.
_
Niambie ni nani umemkutana sana kati ya hawa watano?
#kelvinkibenje
#begood