Aina za Meli

Aina za Meli

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
5,489
Reaction score
14,091
Meli ni chombo ambacho hutumika katika usafiri wa maji na ina uwezo mkubwa wa kubeba watu na mizigo.

Asilimia kubwa ya mizigo hapa duniani kutoka bara moja kwenda bara lingine usafirishwa kwa njia ya meli.

Zifuatazo ni aina mbalimbali za meli na kazi zake.

Meli ya mizigo (Cargo Ship)
Meli hii ubeba mizigo ambayo haipo katika mfumo wa vimiminika kama vile container,ngano,makaa ya mawe na cement.


Meli ya kubeba magari (Ro-Ro)
Inafahamika kama Ro-Ro (Roll on Roll off) hii ni meli ambayo hubeba magari. Hii uwezesha gari kuingia kwa kuendeshwa na kutoka kwa kuendesha hivyo kuepusha matumizi ya kuitoa gari kwa kunyanyuliwa na crane au winch.

Gari hupakiwa kwenye meli na kufungwa ili zisisogee eneo lake pale meli inapokuwa safarini.


Meli ya Mafuta (Tanker)
Hizi hubeba mizigo iliyo katika hali ya kimiminika(liquid form) kama vile mafuta ghafi,petrol,dizeli,mafuta ya taa,gesi,maji na kemikali.


Meli ya Abiria (Passenger Ship)
Meli ya abiria ni ile ambayo uweza kubeba abiria kuanzia 12 na kuendelea. Meli hii ubeba abiria kutoka eneo moja kwenda eneo lingine. Usalama na sheria kali uzingatiwa ili kulinda abiria.

Meli ya Uvuvi (Fishing Vessel)
Meli hii hutumika katika shughuli mbalimbali za uvuvi wa kibiashara.


Meli ziendazo kasi (High speed craft)
Hizi pia hufahamika kama fast ferry, kwa sababu ya kasi zinayotumia kutokana na kutumia engine za jet propela na powerful turbine propeller.


N.B: Meli huweza kuwekwa katika aina kulingana na matumizi mengine ya hiyo meli mfano Tug Boat hizi hutumika kuvuta au kusukuma meli kubwa ziingiapo na kutoka bandarini.
Pilot Boat kuwabeba mapilot wakati wa kufuata na kusindikiza meli.
6-Different-Types-of-International-Ships.jpg
6-Different-Types-of-International-Ships12.jpg
9k%3D.jpg
6-Different-Types-of-International-Ships31.jpg
2Q%3D%3D.jpg
Z.jpg
 
Ivi nyama zinazosafirishwa kutoka USA kwenda China. Wanatumia ndege kubwa au meli?
 
Mheshimiwa Rais, bombardier zinatosha naomba tununue Meli sasa za Taifa
 
Ivi nyama zinazosafirishwa kutoka USA kwenda China. Wanatumia ndege kubwa au meli?
Kwenye meli wanatumia meli ambayo ina mfumo ambao umeunganishwa na system ya refrigeration. Ambazo hizi meli huitwa refeer ship.

Huwa na cold room au bidhaa uwekwa kwenye kontena ambalo lina mfumo wa refrigeration.
 
Mheshimiwa Rais, bombardier zinatosha naomba tununue Meli sasa za Taifa
Kuna meli kubwa mbadala wa Mv Victoria kule Mwanza kuna wa Korea walikuwa wanafanya upembuzi yakinifu wa kuanza kuunda walishinda tenda ya kuunda hiyo meli ya abiria.

Kuna speech ya Rais alipokuwa Bukoba anazindua uwanja wa ndege aliongea kuwa mwaka huu itaanza kuundwa meli hiyo ya abiria.
 
Kwakua panton halijaainishwa kama meli hiyo inamaanisha sijawahi kupanda meli wala ndege tangu nizaliwe.
 
Kwakua panton halijaainishwa kama meli hiyo inamaanisha sijawahi kupanda meli wala ndege tangu nizaliwe.
Umewahi panda meli pantoni nayo ni aina ya meli.

Pantoni au ferry ni aina ya meli. Hii hufanya kazi ya kuvusha watu na magari kutoka eneo moja kwenda eneo lingine ila haiusishi kusafiri kutoka nchi kwenda nchi nyingine au masafa marefu.
 
Back
Top Bottom