Zakaria Maseke
Member
- Apr 26, 2022
- 90
- 150
Kabla ya kuanza biashara, ni muhimu kuchagua muundo unaofaa malengo yako. Muundo wa biashara unaathiri usimamizi, uwajibikaji, ulipaji kodi & ukuaji wa biashara.
Zifuatazo ni aina kuu za miundo ya biashara;
1. BIASHARA YA MTU MMOJA (SOLE PROPRIETOR) - Ni biashara inayomilikiwa na kuendeshwa na mtu mmoja. Mmiliki anapata faida zote na kubeba hasara na madeni yote ya biashara.
2. KAMPUNI (COMPANY) - Ni aina ya biashara inayojitegemea (kutenganishwa) kisheria na wamiliki wake. Faida za kufungua kampuni ni rahisi kuvutia wawekezaji. Inafaa kwa biashara zinazolenga kukua, kuvutia wawekezaji wakubwa au kushiriki zabuni na miradi mikubwa. Sifa za kampuni inaweza kumiliki mali, kuingia mikataba, kushtaki au kushtakiwa kwa jina lake. Wamiliki (wanahisa) wanawajibika kwa kiwango cha hisa walizowekeza. Pia kampuni itaendelea kuwepo hata wanahisa au waanzilishi wakifa au kubadilika.
3. UBIA (PARTNERSHIP) - Ni aina ya biashara inayomilikiwa na watu wawili au zaidi kwa makubaliano. Wabia hugawana faida, hasara na majukumu kulingana na makubaliano yao (mkataba wa ubia).
4. CHAMA CHA USHIRIKA (CO-OPERATIVE SOCIETY) - Ni biashara inayoundwa na kundi la watu wenye lengo la kuboresha maslahi yao ya kiuchumi au kijamii. Wanachama huchangia mtaji na kugawana manufaa kwa mujibu wa sheria na kanuni za ushirika. Mfano SACCOS.
5. TRUST - Ni mfumo wa kisheria ambapo mali hutunzwa au kushikiliwa kisheria na mtu au taasisi (trustee) kwa niaba na manufaa ya watu wengine (beneficiaries) kwa kufuata masharti yaliyowekwa na mwanzilishi wa trust. Mara nyingi hutumika kwa misaada, elimu, dini au usimamizi wa mali.
6. SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI (NON-GOVERNMENTAL ORGANIZATION / NGO) - Ni taasisi inayoundwa kwa lengo la kutoa huduma kwa jamii na kuleta maendeleo, bila lengo la kupata faida kwa waanzilishi au wanachama wake. NGO inaweza kuwa na miradi ya kuzalisha mapato ili kufadhili shughuli zake za kijamii. Hata hivyo, mapato au fedha inayopatikana haigawiwi kwa waanzilishi au wanachama wake kama faida. Badala yake, fedha hizo hutumika kuendeleza na kutekeleza malengo na shughuli za shirika kwa manufaa ya jamii.
Kazi za NGO:
• Kutoa huduma za elimu.
• Kutoa huduma za afya.
• Kutetea haki za binadamu.
• Kuhifadhi mazingira.
• Kuwezesha wanawake, vijana na makundi maalumu.
• Kutoa misaada wakati wa majanga na dharura.
• Kupunguza umaskini kupitia miradi ya maendeleo.
• Kutoa mafunzo na kuongeza uelewa wa jamii kuhusu masuala mbalimbali n.k.
7. VIKUNDI - Ni muunganiko wa watu kwa lengo la kuweka akiba, kukopeshana fedha au kufanya shughuli za maendeleo mfano VICOBA. Vikundi vinaweza kufanya biashara, lakini havitambuliki kama aina ya biashara mpaka visajiliwe.
Kwa ujumla, hakuna muundo mmoja unaofaa kila biashara. Chagua muundo unaoendana na ukubwa wa biashara na malengo yako ya muda mrefu na kiwango cha ulinzi wa kisheria unachohitaji.
Kuchagua muundo sahihi wa biashara kunaweza kukuokoa gharama, migogoro na changamoto za kisheria baadaye.
Je, biashara yako ipo katika muundo gani?
Mwandishi: Zechariah Wakili Msomi
📞 0612275246 / 0754575246 (WhatsApp)