Ngoja nikupe muongozo kidogo tu maana mi mwenyewe nina Ps4 kwahyo sibahatishi huu ushauri naokupa,
Sifa za Ps4 Flat(FAT) ni kwamba yenyewe inakuwa pana kidogo na ina ngazi ila hii kwa matumizi ya nyumbani inafaa na inakula umeme mdogo, udhaifu wake ni kwamba ikitumika muda mrefu huanza kuleta matatizo ya kuchemka kupitiliza na ikichezewa masaa 7 mfululizo hujizima ghafla.
Pia hizi ni bei rahisi kidogo ila kama unataka kufungua biashara sikushauri ununue hizi maan zikishatumika muda mrefu zinaanza matatizo.
Ps4 Slim hili nalijua nje ndan maana nalimiliki, kiufupi hili linaweza tumika hata miaka na halina tatizo lolote,
kwenye upande wa umeme linatumia unit 1.4 likitumika kwa masaa 6 mfululizo bila kuzima hapo ni kama unachezea kwenye Tv isiyo na 4K HD ila kama utatumia TV ya 4K unit zitazidi kidogo mpaka 2 unit hivi 6/hrs.
Ps4 pro hili ni bomba sana kama unapenda Good and smooth graphic ila ukitaka kulienjoy hili inabidi uwe na TV ya 4K ndo utafaidi hili game tofauti na hapo ina view kama Ps slim na Fat tu, udhaifu wake yenyewe ni kwenye umeme tu hili linakula sana umeme ila kwenye ubora ni zuri sana.
Kuhusu upande wa Chipped na non-chipped kuanzia version 9 linaweza kuwa chipped ila kuanzia version 11 kwenda juu haiwezekani kuwa chipped, kwa ushauri tu nakushauri bora upate lililo chipped maan sio gharama kupata magemu yake ila ukiwa na non chipped game lake moja ni mpka 65k wakati chipped kwa 25k unaweza kupata game.
Ps non chipped uzuri wake ni kwamba utaweza kuingia online na kuangalia hata Netflix na inaingia internet kama Pc tu na kama upo vzuri kifedha unaweza kuwa unadownload magemu mwenyew tu,
Ps chipped hili kinachofanyika ni kuvunja software isiwe na access ya internet yani sawa na kuiondoa kwenye server za internet kwahyo games zake zitaingizwa kwa mfumo kama wa (Apk + obb ya kwenye simu) hasara yake ni kwamba tu hutopata access ya internet na hutoweza kudownlod games online, na pia hutoweza ku update version ya Ps lako kama itatoka.
So kwa upande wangu mimi ninalo (Ps4 Slim non-chipped) ila changamoto nayopata ni kupata games tu maan ni bei ghali kidogo, kila kitu unacheza offline ila ukitaka kucheza na watu wengine Duniani ndo utawasha Data ili ucheze nao,
Kwa ushauri mi nakushauri tu ununue Ps4 slim na hili ndo pendekezo kubwa linalotolewa na watu wengi wenye Ps maan kwanza ni imara unaweza kulitumia miaka na pia linatumia umeme mdogo usinunue Flat(FAT) na kwakuwa unataka kuchezesha pia sikushauri ununue Ps4 pro maana linakula sana umeme, kama una swali niulize.