Aina za Presha ya Kushuka na Sababu ya tatizo hilo

Aina za Presha ya Kushuka na Sababu ya tatizo hilo

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
AINA ZA PRESHA YA KUSHUKA

Kuzifahamu aina kuu nne za presha ya kushuka (hypotension) husaidia kujitambua au kutambua hali ya mgonjwa.

1. Postural or orthostatic hypotension (OH):
Ni aina ya kushuka kwa presha ambayo hutokea mara baada ya mtu kusimama haraka. Aina hii hutegemea umri wa mtu husika, mara nyingi 5% hadi 11% ni umri wa kati na 30% au zaidi kwa wazee.

2. Postprandial hypotension:
Aina hii ya presha kushuka hutokea mara baada ya kula chakula. Utumbo huhitaji damu nyingi kwaajili umeng’enyaji. Aina hii ya presha ya kushuka ndio ambayo hutokea zaidi kuliko aina ya kwanza hapo juu na hutokea kwa wazee zaidi. Magonjwa yanayoathiri mfumo wa fahamu mkuu kama Parkinson disease na autonomic neuropathy.

Dawa kama octreotide hupunguza kiwango cha damu kwenye utumbo. Baadhi ya dawa za maumivu hupelekea kukusanyika kwa chumvi mwilini hatimae kuongeza kiwango cha famu mwilini.

3. Neurally mediated hypotension:
Aina hii ya presha kushuka hutokea mara baada ya kusimama kwa muda mrefu.

4. Multiple system atrophy with orthostatic hypotension:
Aina hii hutokea mara baada uharibifu wa mfumo wa fahamu ufahamikao kama autonomic nervous system, hali hii hipelekea presha wakati wa kusimama na presha ya kupanda wakati wa kulala.


SABABU ZA PRESHA YA KUSHUKA

20210713_191801_0001.png

Kila mtu anaweza kukutwa na presha ya kushuka, hasa waliopo katika umri wa miaka 65. Hali zifuatazo na uchukuaji wa baadhi ya dawa unaweza kuhatarisha uwezekano wa kuugua presha ya kushuka.

1. Upungufu wa maji mwilini:
Licha ya kiwango kidogo cha upungufu wa maji husababisha presha ya kushuka. Kupungua kwa maji mwilini hutokana na kupatwa na kichefu chefu, kutapika au kuharisha sana kwa muda mrefu. Katika hali hii, maji mengi hupotea.

Wagonjwa wenye upungufu wa maji kidogo wanaweza kukutwa na hali ya kiu na mdomo kuwa mkavu. Kwa mwenye upungufu wa maji wa wastani inaweza kusababisha presha ya kushuka na upungufu wa maji mkubwa husababisha kufeli kwa figo, kuchanganyikiwa, kupoteza uwezo wa kuhisi sehemu za mwili, na hatimae kifo.

2. Upotevu wa damu mwilini:
Jeraha kubwa la nje au kuvuja kwa damu nyingi kunaweza kusababisha presha ya kushuka. Kuvuja kwa damu kunaweza kutokea mara baada ya jeraha kubwa, ajali, magonjwa ya mfumo wa utumbo.

3. Matatizo ya moyo:
Matatizo yanayohusianana valvu za moyo kama “aortic stenosis”, msukumo wa damu kupungua, mshituko wa moyo, na baadhi ya matumizi ya dawa ambazo zenye madhara kwenye moyo, na misuli ya moyo kuathiriwa na magonjwa kama virusi.

Mapigo ya moyo kupungua hupelekea presha ya damu kupungua, kizunguzungu na hatimae kupoteza fahamu. Sababu zinazopelekea mapigo ya moyo kupungua ni kama matatizo ya moyo na dawa aina ya digoxin kuzidi (digoxin toxicity).

4. Matatizo ya aleji mwilini
Aina hii ya aleji hutokana na uzalishwaji wa kemikali ijulikanayo kama immunoglobulin E ambayo hupelekea kushuka haraka kwa presha.

5. Kuathirika kwa kongosho (Pancreatitis):
Kongosho ilioathiriwa husababisha maji mengi kutoka sehemu ya mishipa ya damu na kwenda kwenye tishu zilizoathiriwa, hatimae kupelekea ujazo wa damu kupungua.

6. Kuathiriwa na baadhi ya magonjwa:
Kuathiriwa na bakteria aina ya gram - negative, na mdudu yoyote akiingia katika mzunguko wa damu hupelekea kushuka kwa kiasi kikubwa cha presha mwilini.

7. Matatizo kwenye mfumo wa homoni mwilini (Endocrine problems):
Ufanyaji kazi zaidi au kidogo wa tezi ya thyroid husababisha presha ya kushuka. Ugonjwa wa kisukari na magonjwa mengine yanayoyokana na homoni kutokuwa sawa.

8. Ujauzito:
Mwanamke mjamzito hukumbwa na hali hii ya presha kushuka kwasababu mahitaji mzunguko wa danu huongezeka zaidi wakati wa ujauzito. Ingawa presha hurudi katika hali yake ya kawaida baada ya kujifungua.

9. Matumizi ya dawa:
Dawa zenye kuongeza utoaji maji mwilini kwa njia ya mkojo (diuretics), dawa zote za presha ya kupanda, dawa zinazohusika katika matibabu ya parkison (Carbidopa na levodopa), dawa aina ya sildenafil endapo ikitumika kwa pamoja na nitroglycerin hupelekea presha ya kushuka.
 
Shukrani kwa elimu, mie inanisumbua sana, nikiwa na hasira, period au mawazo,

Natamani nipate dawa yake iishe kabisa.
 
mimi nikinywa chai asubuhi lazma moyo niusikie tofauti yaani mapigo yanazidi halafu najiskia vibaya
 
Back
Top Bottom