Air Seychelles kuzindua njia mpya Dar es Salaam

Air Seychelles kuzindua njia mpya Dar es Salaam

Kozo Okamoto

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2013
Posts
3,391
Reaction score
1,545
AIR-seychelles.jpg


Air Seychelles kuzindua njia mpya Dar
Shirika la Ndege la Jamhuri ya Shelisheli, ‘Air Seychelles' liinatarajia kuzindua safari za ndege zake jijini Dar es Salaam Desemba 2 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Air Seychelles, Manoj Papa, Tanzania kupitia Jiji lake la Dar es Salaam, inakuwa ni ya tatu kwa ndege zao kufanya kazi, kupitia mtandao wa ukanda wa bahari ya Hindi baada ya Mauritius na Johannesburg.

Alisema njia hiyo mpya itakuwa na ndege ya kisasa Airbus A320 Aircraft yenye madaraja mawili likiwemo la biashara lenye viti 16 na uchumi viti 120.

"Kwa sasa lengo letu ni kuhakikisha tunajenga nguvu kubwa katika mtandao wa kimataifa, katika huduma za usafirishaji kwa kufungua milango ya kibiashara ndani ya bara la Afrika," alisema Papa na kuongeza.

Jiji la Dar es Salaam linalokuwa kwa kasi katika nyanja za kibiashara na utalii, kutaongeza muingiliano mkubwa wa kisoko kwa mataifa yote inapopita ndege hiyo, ikiwemo nchi ya Shelisheli.

Ndege hiyo pia itakuwa msaada mkubwa kwa wateja mbalimbali, ikiwemo kuwaunganisha na Abu Dhabi na mataifa mengine mengi yaliyopo ndani ya Bara la Hindi.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya ndani na Usafirishaji, Joël Morgan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Air Seychelles, alisema njia hiyo mpya itasaidia fursa za kiuchumi kwa kufungua milango ya kibishara na utalii.


Chanzo: Tanzania Daima
 
Huu ni mwanzo mzuri sana hasa kwa Sector ya Utalii.
Nchi hiyo ina Beach bomba sana,sasa itakuwa ni nafasi nzuri kwa wageni wanaotoka huko kuja Tanzania kwa ajili ya Safaris za kutemebelea mbuga za wanyama.
Na pia itafanya pia wageni wanaotoka Kutembelea mbuga za wanyama kwenya Kwao kwa ajili ya fukwe nzuri.
Inakuwa Give and take.Ila hofu tu kwamba kwa Upande wa Zanzibar ikiingiza vurugu za uchaguzi basi hawa wata take advantage ya Beach Holidays kwakuwa na connection ya uhakika.
Hatua nzuri sana
 
Ni hatua nzuri kibiashara kwa upande wa Bara , ila kwa Zanzibar ni mwiba mkali. Seychelles ni nchi pekee barani Africa yenye Beach nzuri. So kitalii Zanzibar itaathirika maana itakuwa rahisi kwa Watalii kuja Safari tour Bara then na kuunga direct flight to Seychelles.
 
Back
Top Bottom