Air Tanzania among entities that borrowed money without approval, says PAC

Mimi niliingia ccm na nilishatoa sababu zangu, Lengo ni kunyoosha mambo binafsi ya biashara ndio lengo kuu

Sikwenda ccm kufuata siasa za ujamaa mimi

Mimi sio mjamaa, Nafanya biashara na mabepari

Hivyo pale ambapo naona nitapata pesa na kulinda pesa napaheshimu sana

Naheshimu ccm kwa kuwa bila ccm ningepata usumbufu wanopata baadhi ya watu wanaotumia akili

Jifanye lofa na mpumbavu kufanikisha mambo yako, Elimu ni makaratasi tu tunayopata darasani

Nina Hakika kuna muda yakupasa kuweka akili mfukoni ili upate pesa mkuu

Wenye Mamlaka ni ccm, Wewe nani upingane na aliyeshika makali

Siwezi kuharibu kazi na Biashara zangu kisa kuwatetea watanzania ambao hawajielewi

Siku wakijielewa na Mimi nitapiga u turn kuwa unga mkono, Hata wewe nitakuunga mkono mkibadilika
 
Sio wewe tu
 
Watu hawasomi ripoti hawaelewi Atcl wanaowadai ni serikali kupitia wakala wa ndege za serikali
 
Who determines hawa waumie, wale wasiumie? Hakuna asiyeheshimu mamlaka, ila kuheshimu mamlaka haina maana kujifedhehesha na kupoteza utu wako! Ujasiri haujawahi kupitwa na wakati
 
Una uhakika kwamba imepewa ridhaa na wananchi?
 
Ni kweli,Ila ukweli ni kwamba hakuna upinzani wa kuupa nchi
Ni ujinga tuu mmejingea kwenye mavichwa yenu eti kwamba nchi nzima haina upinzani wakati daily mnaona mambo mabaya na mateso wanayoyapata wapinzani.
 
Uko sahihi

ATCL haikopesheki kabisa

Ripoti ya CAG imepotoka ilitakiwa itamke wazi bila kumumunya maneno kuwa serikali ndio ilikopa kununua ndege

CAG kwa nini anasukumia zigo kwa ATCL? Wakati ndege zile mpya zote ni mali ya serikali sio ATCL? Yaani serikali ikope ndege zisomeke hati kwa jina la serikali halafu zigo asukumiwe ATCL SIO SAHIHI

Mkaguzi wa serikali hiyo ripoti akaiandike upya
 
AICC inafanya biashara gani mpaka ikope pesa, ni vyema AICC ikodishwe kwa mwekezaji toka nje ya Afrika au Uarabuni.
AICC ipo ipo tu kimkakati kulinda ajira za watu pale lakini kimsingi hakuna ufanisi kwenye taasisi ile. Rwanda ndio imechukua majukumu ya AICC kwa sasa na hii ni baada ya kuona AICC inapwaya sana.
Hivi kulikuwa na sababu gani ya kujenga ukumbi mwingine wa JNICC kama tawi la AICC badala kuiboresha? Ikumbukwe Nairobi waimezea mate hiyo keki ikiwemo kutaka makao makuu ya Jumuia ya Afrika Mashariki. Hivi watanzania huwa tunafeli wapi?.
 
Unachokisema ni kweli ... Mashirika haya yenye high risk in terms of operation inabidi kuwe na mtaalamu kabisa lets say hata rubani mstaafu
 
Hii njemba huwaga ni kiazi......
inajua kulia lia tu.....
mkewe atakuwa na tabu sana manake ni nyenye
 
P.msimamizi wa serikali ni bunge au ni nani na kamani bunge hilo bunge limetokana na chama gani.ni kweli serikali ni mtekelezaji lkn hiyo serikali imeundwa na nani?
 
Tatizo tunaamua tu kufuata ushabiki wa vyama kama misukule. Precision amekuwapo miaka nenda rudi hivi nchi imesogea wapi katika usafiri wa anga? ATCL sasa hivi wanatupeleka mikoani na nchi za nje na sio kikombe cha kujazia maji mtungi wa Kenya Airways. Nafikiri swala lakutilia mkazo ni jinsi ATCL inavyotakiwa kuendeshwa ili iwe na tija na si vinginevyo. Kinyume chake tutabaki gulio la nchi nyingine. Angalia Ilani za CCM, UKAWA/CHADEMA na ACT Wazalendo za mwaka 2015 kuhusu ATCL ndio utaelewa Watanzania ni misukule. Ilani zao za mwaka 2020 hawakugusia kabisa ATCl kwa sababu tayari Magu alishamaliza!

Kwa hiyo ukijaribu na kufeli mara moja au mara kumi then unabaki kulia tu au kujifunza nini makosa yako na kujaribu tena? Kama alivyosema Paschal, nadhani huyu Makamu Mwenyekiti wa PAC hana hata ufahamu wa ATCL pamoja na kwamba alikuwa Waziri maana tunaambiwa ATCL sio wamiliki wa ndege kwa hiyo swala la kukopa ni Serikali kama lipo maana tuliambiwa ndege ni cash purchasing. Hapo inabidi tujiulize kama huyu aliyekuwa katika baraza la mawaziri hajui hili basi kama wengi wanvyosema kulikuwa na issue ya Governance kama alivyosema Katibu mkuu Kiongozi siku ya kuapishwa kwake au ambavyo Mama Samia amekuwa akisisitiza kuhusu kuondoa vibanda ndani ya Serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…